TEMBELEA: www.sokainbongo.com
Ghana 1 Australia 1
Ghana wameweza kutoka sare 1-1 na Australia ambayo katika mechi yake ya pili mfululizo wamelazimika kucheza wakiwa pungufu baada ya leo Straika wao Harry Kewell kupewa Kadi Nyekundu kwa kuushika mpira uliokuwa ukitinga wavuni yeye akiwa kasimama mstari wa golini.
Katika mechi ya kwanza na Germany Mchezaji Tim Cahill alipewa Kadi Nyekundu.
Australia ndio walioanza kupata bao dakika ya 11 kupitia Holman baada ya Kipa Kingson kuitema frikiki ya Bresciano na mpira kumaliziwa na Holman.
Ghana walipewa penalti dakika ya 25 na Asamoah Gyan akaifungia Ghana bao la kusawazisha hii ikiwa ni penalti yake ya pili kwani katika mechi ya kwanza na Serbia aliipa ushindi wa 1-0 kwa penalti.
Penalti hiyo ya Ghana ilitokea baada ya Harry Kewell kuzuia shuti la Annan kwa mkono akiwa mstari wa goli na Refa Roberto Rosetti kuamua penalti na kumpa Kadi Nyekundu Kewell.
Kwa sare ya leo Ghana wametua kilele cha Kundi D wakiwa na pointi 4, Germany pointi 3, Serbia pointi 3 na Australia 1
Timu:
Ghana: Kingson; Pantsil, Jonathan Mensah, Addy, Sarpei; Annan; Asamoah, Boateng; Ayew, Gyan, Tagoe.
Australia: Schwarzer; Wilkshire, Moore, Neill, Carney; Valeri, Culina; Emerton, Holman, Bresciano; Kewell.
Refa Roberto Rossetti.
Uholanzi waiua Japan
Uholanzi imejiweka nafasi nzuri ya kutinga Raundi ya Pili ya Kombe la Dunia walipoifunga Japan bao 1-0 katika mechi ya Kundi E huko Mjini Durban Uwanja wa Moses Mabhida iliyochezwa leo Jumamosi Juni 19.
Uholanzi walishinda mechi yao ya kwanza wa bao 2-0 dhidi ya Denmark na Japan walifunga Cameroun 1-0.
Uholanzi watapata uhakika wa kusonga mbele ikiwa katika mechi nyingine ya Kundi E itakayochezwa baadae leo Cameron watashindwa kuifunga Denmark.
Bao la ushindi kwa Uholanzi alifunga Wesley Sneijder dakika ya 52.
Anelka afungishwa virago kurudishwa kwao!!
Straika wa Ufaransa anaechezea Chelsea huko England, Nicolas Anelka, anadaiwa kumtukana Kocha wa Ufaransa, Raymond Domenech, katika tukio ambalo limetokea wakati wa mapumziko kwenye mechi ya juzi Alhamisi Ufaransa waliyofungwa 2-0 na Mexico.
Inasemekana Domenech alimlaumu Anelka kwa kutokuwa makini na pozisheni yake na ndipo Anelka akalipuka na kumtukana Kocha huyo matusi ya nguoni.
Domenech akambadilisha Anelka na kumuingiza Andre-Pierre Gignac
kabla Kipindi cha Pili kuanza.
Kumekuwa na madai ya kuwa kambi ya Timu ya Ufaransa haiko shwari na kumekuwa na mpasuko mkubwa ingawa Viongozi wamekuwa wakikanusha hilo.
Ufaransa wanamaliza mechi zao kwa kucheza na Afrika Kusini siku ya Jumanne Juni 22 na Mexico na Uruguay wanacheza pamoja siku hiyo hiyo na wanahitaji sare tu ile wote wawili wasonge mbele.
No comments:
Post a Comment