CHEKI: www.sokainbongo.com
England yabanwa mbavu
Inabidi England waifunge Slovenia katika mechi yao ya mwisho ikiwa watataka kusonga Raundi ya Pili ya Kombe la Dunia baada ya kutoka sare 0-0 na Algeria Uwanja wa Green Point huko Cape Town.
England walicheza chini ya kiwango na kushindwa kufunga bao.
Baada ya mechi Timu hiyo ilizomewa na Mashabiki wao wenyewe na hata Kocha wao, Fabio Capello, alilalamika: “Haikuwa Timu ninayoijua mimi, Timu ninayoiona mazoezini.”
Katika Kundi C, Slovenia wanaongoza wakiwa na Pointi 4, USA 2, England 2 na Algeria 1.
Mechi za mwisho hapo Juni 23 ni Slovenia v England na Algeria v USA.
Timu:
England: James, Johnson, Carragher, Terry, Ashley Cole, Lennon,
Barry, Lampard, Gerrard, Rooney, Heskey.
Akiba: Green, Dawson, Crouch, Joe Cole, Warnock, Upson, Milner, Wright-Phillips, Defoe, King, Carrick, Hart.
Algeria: M'Bohli, Bougherra, Belhadj, Yahia, Kadir, Yebda,
Lacen, Halliche, Boudebouz, Ziani, Matmour.
Akiba: Gaouaoui, Mansouri, Ghezzal, Saifi, Djebbour, Bellaid, Laifaoui,
Guedioura, Medjani, Mesbah, Abdoun, Chaouchi.
Refa: Ravshan Irmatov (Uzbekistan)
TOSIC: ‘MKOPO UNGEFAA!’
Zoran Tosic amedai Sir Alex Ferguson hakumpa nafasi ya kutosha alipokuwepo Manchester United na ndio maana akashindwa kuonyesha makeke yake.
Winga huyo kutoka Serbia ameuzwa kwa CSKA Moscow ya Urusi baada ya kukaa Old Trafford Miezi 18 tu na kucheza mechi 5 ambazo zote alitokea benchi.
Msimu uliokwisha Tosic alipelekwa Bundesliga kucheza kwa mkopo Klabu ya Cologne.
Tosic amelalamika kuwa bora angpelekwa CSKA kwa mkopo na si kuuzwa moja kwa moja
No comments:
Post a Comment