Wednesday 16 June 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Spain chaliiii!!
Hawajafungwa muda mrefu na wengi walikuwa tayari wamewakubali kuwa Spain ndio Mabingwa wa Dunia watarajiwa lakini leo Jumatano Juni 16 katika mechi yao ya kwanza ya Kundi H katika Fainali za Kombe la Dunia iliyochezwa Uwanja wa Moses Mabhida, Durban, Spain wamepigwa bao 1-0 na Uswisi.
Matokeo haya ndio makubwa ya kustua yaliyotokea tangu kuanza Fainali hizi kwani Spain, mbali ya kushabikiwa kuwa Bingwa wa Dunia, katika mechi 48 za mwisho alizocheza kabla ya leo ameshinda 45 kati ya hizo.
Ilikuwa ni dakika ya 52 ndio iliyowaliza Spain pale goli kiki ndefu ya Uswisi ilipomkuta Derdiyok aliepiga kwa kichwa kwa Nkufo na kuchomoka kuomba tena mpira akiwa katikati ya Madifenda wa Spain Pique na Puyol na ndipo Kipa Casillas akaruka miguu mbele na kumwangusha Derdiyok lakini Refa hakusimamisha mpira na mpira huo ukamgonga Pique na kutiririka kwa Fernandez aliupachika wavuni.
Timu:
Spain: 1-Iker Casillas; 15-Sergio Ramos, 3-Gerard Pique, 5-Carles Puyol, 11-Joan Capdevila; 16-Sergio Busquets; 8-Xavi, 14-Xabi Alonso; 21-David Silva, 7-David Villa, 6-Andres Iniesta.
Switzerland: 1-Diego Benaglio; 13-Stephane Grichting, 2-Stephan Lichtsteiner, 4-Philippe Senderos, 17-Reto Ziegler; 7-Tranquillo Barnetta, 8-Gokhan Inler, 6-Benjamin Huggel, 16-Gelson Fernandes; 19-Eren Derdiyok, 10-Blaise Nkufo.
Refa: Howard Webb (England)
Ratiba 2010/11 Ligi Kuu England kesho!!!
Klabu za Ligi Kuu England kesho Alhamisi Juni 17 zitajua ratiba zao kwa Msimu mpya wa 2010/11 utakaoanza Agosti 14.
Kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu kutakuwa na lile pambano la fungua pazia la Ngao ya Hisani litakalochezwa Uwanja wa Wembley hapo Agosti 8 kati ya Mabingwa wa Ligi Kuu na Kombe la FA, Chelsea, dhidi ya Manchester United ambao walishika nafasi ya pili kwenye Ligi.
Capello anatafakari mabadiliko
Kocha wa England Fabio Capello amedokeza Kiungo Gareth Barry ataanza mechi na Algeria Siku ya Ijumaa baada ya kupona enka lakini bado hajaamua nani atakuwa patna wa Wayne Rooney kwenye mashambulizi.
Pia baada ya kufanya kosa kubwa kwenye mechi ya kwanza na USA na kufungisha bao lililowapa sare ya 1-1 USA, Kipa Robert Green hana uhakika kama atacheza mechi hiyo na Algeria.
Rooney bado ana matumaini
Mshambuliaji wa England, Wayne Rooney, bado ana matumaini ya kufanya vizuri kwenye Kombe la Dunia licha ya kwenda sare na USA ya 1-1 katika mechi ya kwanza ya Kundi C.
Kuhusu yeye fomu yake ya ufungaji kudidimia ambayo amefunga bao moja tu katika mechi 8 za mwisho za  Kimataifa za England, Rooney amesema hilo halimtii hofu mradi tu wengine wanafunga na England inashinda.
Rooney pia amemponda Mkongwe wa Ujerumani Franz Beckenbauer aliedai England inacheza butua na kukimbiza mpira tu kwa kusema: “Hayo ni maoni yake! Sisi hatuko hivyo na hatusikiliza vitu hivyo.”

No comments:

Powered By Blogger