Sunday 13 June 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Capello na utata wa Kipa!!!
Meneja wa England Fabio Capello ana mtihani mkubwa wa kuchagua nani Kipa wake katika mechi ijayo ya Kombe la Dunia England v Algeria Ijumaa Juni 18 baada ya Kipa aliekuwa akimtegemea Robert Green kuiangusha vibaya kwa kutoa goli la zawadi kwa USA na kufanya mechi imalizike 1-1.
Makipa wengine wa England ni Mkongwe David James na Chipukizi Joe Harta mbao wote hao ni mahiri na kwa baadhi ya Wadau ni, pengine, bora kupita Robert Green.
Capello amekataa kumlaumu Green lakini ameweka bayana hajaamua nani atakuwa Kipa kwenye mechi na Algeria.
Capello amesema: “Makosa ni makosa, nitaongea na Green na baada ya hapo nitaamua.”
Argentina v Nigeria walengwa na Mionzi ya Leza kwenye mechi
FIFA imeamuru ufanyike uchunguzi wa kina baada ya Wachezaji kwenye mechi kati ya Argentina na Nigeria kulengwa na Mionzi ya Kijani toka kwenye Leza Uwanjani Ellis Park, Johannesburg hapo jana.
Ingawa hamna Timu iliyolalamikia tukio hilo, FIFA imeamua kulichunguza ili kujua Mtu huyo alipitapita vipi na chombo cha kulengesha Mionzi ya Leza na kuingia ndani ya Uwanja.
Mara baada ya kugundulika Mionzi hiyo Walinzi walifuatilia na haikurudiwa tena.
Hii si mara ya kwanza kwa Mionzi ya aina hiyo kutumika Uwanjani kwani Februari 2008 Cristiano Ronaldo alipokuwa akiichezea Manchester United dhidi ya Lyon huko Ufaransa alilengwa nayo kwenye mechi hiyo.

No comments:

Powered By Blogger