Thursday 17 June 2010

ANGALIA: www.sokainbongo.com

Nigeria wajinyonga!!
Ugiriki leo wameifunga Nigeria bao 2-1 baada ya kutoka nyuma kwa bao 1-0 lakini ni Nigeria wenyewe ndio waliosababisha hali hiyo baada ya wenyewe kujitia kitanzi pale Mchezaji wao Sani Kaita alipotwangwa Kadi Nyekundu dakika ya 33 kwa kumrushia teke Katsouranis ambae licha ya teke hilo kutokumgusa vilivyo alijidondosha chini mithili amelipuliwa na bomu.
Ushindi huu wa Ugiriki umewaweka Nigeria kwenye hali ngumu mno na pengine ni miujiza mikubwa itakayowafanya waingie Raundi ya Pili kwani wameshafungwa mechi mbili na wamebakisha moja tu na Korea Kusini huku Ugiriki na Korea Kusini kila moja zina pointi 3 na vinara ni Argentina wana pointi 6 baada ya kushinda mechi zao mbili.
Ugiriki watamaliza na Argentina.
Katika mechi hii Nigeria walipata bao dakika ya 16 kupitia Uche ambae frikiki yake ilienda moja kwa moja wavuni huku Kipa Tzorvas akidaivu mbovu.
Ndipo wehu wa Kaita kwenye dakika ya 33 wa kurusha teke kumfanya atolewe nje na kuiacha Nigeria iwe Mtu 10.
Hapo ndipo Kocha wa Ugiriki akapata mwanya na kumtoa Beki mmoja na kumuingiza Straika na Ugiriki ikaanza wimbi baada ya wimbi kutafuta bao la kusawazisha na dakika ya 44 shuti la Salpingidis likamgonga Haruna na Kipa Enyeama akapangua lakini mpira ukarudi tena kwa Salpingidis aliefumua shuti wavuni.
Bao la ushindi kwa Ugiriki lilipatikana kufuatia Kipa Enyeama kutema shuti la Karagounis na mpira kumdondokea Torosidis aliefunga.
Timu:
Greece: 12-Alexandros Tzorvas; 11-Loukas Vyntra, 16-Sotiris Kyrgiakos, 15-Vassilis Torosidis, 6-Alexandros Tziolis, 8-Avraam Papadopoulos, 19-Socratis Papastathopoulos, 10-Giorgos Karagounis, 21-Kostas Katsouranis; 14-Dimitris Salpingidis, 17-Fanis Gekas.
Nigeria: 1-Vincent Enyeama; 17-Chidi Odiah, 6-Danny Shittu, 2-Joseph Yobo, 3-Taye Taiwo, 12-Kalu Uche, 20-Dickson Etuhu, 15-Haruna Lukman, 14-Sani Kaita, 8-Yakubu Aiyegbeni, 11-Peter Odemwingie.
Refa: Oscar Ruiz (Colombia)

No comments:

Powered By Blogger