Friday 11 December 2009

LIGI KUU ENGLAND:
JUMAMOSI, 12 Desemba 2009
Birmingham v West Ham
Bolton v Man City
Burnley v Fulham
Chelsea v Everton
Hull v Blackburn
Man Utd v Aston Villa
Stoke v Wigan
Sunderland v Portsmouth
Tottenham v Wolverhampton
JUMAPILI, 13 Desemba 2009
Liverpool v Arsenal
MCHEZAJI BORA AFRIKA: Wachezaji watano watajwa kugombea!!
Samuel Eto'o, aliewahi kushinda Tuzo ya Mchezaji Bora Afrika mara 5, na Didier Drogba, alieshinda mara moja, wamo kwenye listi ya Wachezaji watano wanaogombea Tuzo hiyo na Mshindi atatangazwa huko Senegal mwezi Februari.
Listi ni:
-Samuel Eto'o [Inter Milan]
-Didier Drogba [Chelsea]
-Michael Essien [Chelsea]
-Yaya Toure [Barcelona]
-Seidou Keita [Barcelona]

Thursday 10 December 2009

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: Arsenal, Liverpool zafungwa, Barca, Inter zasonga!!
Timu za England, Arsenal na Liverpool, jana zilifungwa kwenye mechi zao za mwisho za UEFA CHAMPIONS LEAGUE.
Ingawa Arsenal alifungwa 1-0 na Olympiacos, ambayo kwa ushindi huo imejihakikishia kuingia Raundi ya Pili, Arsenal tayari waliwakuwa washafuzu kuingia Raundi hiyo ya Pili na pia kuwa kiongozi wa Kundi lao. Hivyo, katika mechi hiyo isiyokuwa na maana, Arsenal walichezesha Wachezaji makinda.
Liverpool, ambao tayari walikuwa washabwagwa nje ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE na kutupwa kwenye EUROPA LIGI kwa vile wamemaliza nafasi ya 3 kwenye KUNDI lao, walifungwa na Fiorentina uwanja wa Anfield mabao 2-1 na hivyo kuihakikishia Fiorentina uongozi Kundi E.
Mabingwa Watetezi Barcelona waliifunga Dynamo Kiev 2-1 na kufuzu kuingia Raundi ya Pili huku wenzao Kundini Inter Milan pia wakiungana nao baada ya kuichapa Rubin Kazan 2-0.
Droo ya kuamua Timu zipi zinakutana Raundi ya Pili itafanyika Desemba 18 na mechi za Raundi ya Pili zitakazochezwa kwa Mtoano, nyumbani na ugenini, zitachezwa Februari 2010.
TIMU ZILIZOFUZU KUINGIA RAUNDI YA PILI BAADA YA MECHI ZA JANA:
KUNDI E:
-Fiorentina
-Lyon
KUNDI F:
-Barcelona
-Inter Milan
KUNDI G:
-Sevilla
-Stuttgart
KUNDI H:
-Arsenal
-Olympiacos
MATOKEO KAMILI MECHI ZA JUMATANO, 9 Desemba 2009
Dynamo Kiev 1 v Barcelona 2
Inter Milan 2 v Rubin Kazan 0
Liverpool 1 v Fiorentina 2
Lyon 4 v Debrecen 0
Olympiakos 1 v Arsenal 0
Sevilla 1 v Rangers 0
Standard Liege 1 v AZ Alkmaar 1
VfB Stuttgart 3 v Unirea Urzicen 1
TIMU ZOTE ZILIZOFUZU KUINGIA RAUNDI YA PILI:
KUNDI A:
-Bordeaux
-Bayern Munich
KUNDI B:
-Man U
-CSKA Moscow
KUNDI C:
-Real Madrid
-AC Milan
KUNDI D:
-Chelsea
-FC Porto
KUNDI E:
-Fiorentina
-Lyon
KUNDI F:
-Barcelona
-Inter Milan
KUNDI G:
-Sevilla
-Stuttgart
KUNDI H:
-Arsenal
-Olympiacos
TIMU ZILIZOMALIZA NAFASI YA 3 KWENYE MAKUNDI NA HIVYO KUINGIZWA EUROPA LIGI:
-Juventus
-Wolfsburg
-Marseille
-Apoel Nicosia
-Liverpool
-Rubin Kazan
-Unirea Urziceni
-Standard Liege

Wednesday 9 December 2009

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: Kipondo cha nyumbani chaitupa nje Juve!!
Man U ya kuungaunga yabonda huko Ujerumani!!!
Bayern Munich, wakicheza ugenini huko Italia, jana waliishindilia Juventus mabao 4-1 na kuitupa nje ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE.
Huko Ujerumani, Manchester United ikichezesha Timu ya kushangaza huku Difensi yao ikilindwa na Wachezaji viungo Park, Fletcher na Carrick wakisaidiwa na Beki wa kawaida Evra ambae jana alivikwa Unahodha, waliibamiza Wolfsburg 3-1 huku mabao yote yao yakifungwa na Michael Owen.
Timu zilizofuzu kusonga Raundi inayofuata ni:
KUNDI A:
-Bordeaux
-Bayern Munich
KUNDI B:
-Man U
-CSKA Moscow
KUNDI C:
-Real Madrid
-AC Milan
KUNDI D:
-Chelsea
-FC Porto
MATOKEO MECHI ZA Jumanne, 8 Desemba 2009
Atletico Madrid 0 v FC Porto 3
Besiktas 1 v CSKA Moscow 2
Chelsea 2 v Apoel Nicosia 2
FC Zurich 1 v AC Milan 1
Juventus 1 v Bayern Munich 4
Maccabi Haifa 0 v Bordeaux 1
Marseille 1 v Real Madrid 3
Wolfsburg 1 v Man Utd 3
MECHI ZA LEO JUMATANO, 9 Desemba 2009
Dynamo Kiev v Barcelona
Inter Milan v Rubin Kazan
Liverpool v Fiorentina
Lyon v Debrecen
Olympiakos v Arsenal
Sevilla v Rangers
Standard Liege v AZ Alkmaar
VfB Stuttgart v Unirea Urzicen

Tuesday 8 December 2009

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: Real, Juve, AC Milan na Bayern kusonga leo?
Klabu vigogo huko Ulaya, Real Madrid, Juventus, AC Milan na Bayern Munich, ambao wote washawahi kuwa Mabingwa wa Ulaya, leo wanacheza mechi zao za mwisho za Makundi yao huku wote bado hawana uhakika wa kuingia Raundi inayofuata.
Rea Madrid, wanaocheza ugenini na Marseille, wana afueni kwani wanaweza kufungwa hata goli 3 na kusonga mbele wakati AC Milan lazima waifunge FC Zurich ili wasonge mbele.
Bayern Munich wanasafiri kwenda Italia kucheza na Juventus na lazima washinde huku Juve wakihitaji suluhu tu.
Klabu za England, Manchester United na Chelsea, tayari zishafuzu kuingia Raundi inayofuata na leo wanamaliza mechi zao kwenye Makundi yao, na ili wajihakikishie kuwa vinara wa Makundi hayo, wanahitaji angalau sare tu.
RATIBA MECHI ZA LEO Jumanne, 8 Desemba 2009
Atletico Madrid v FC Porto
Besiktas v CSKA Moscow
Chelsea v Apoel Nicosia
FC Zurich v AC Milan
Juventus v Bayern Munich
Maccabi Haifa v Bordeaux
Marseille v Real Madrid
Wolfsburg v Man Utd
UKOSEFU WA MADIFENDA MAN U: Kinda wa Bosi aingizwa Kikosini!!
Oliver Gill, umri miaka 19, ambae ni mtoto wa David Gill, Mkurugenzi Mtendaji wa Manchester United, amechukuliwa kwenye Kikosi cha Timu hiyo ambayo leo usiku ipo Ujerumani kupambana na Wolfsburg kwenye mechi ya mwisho ya Kundi lao kwenye mashindano ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE.
Man U washafuzu kuingia Raundi inayofuata lakini wanahitaji sare ili wajihakikishie uongozi wa Kundi lao na pengine kupata unafuu wa kupangiwa mpinazini dhaifu Raundi inayofuata.
Wolfsburg, ili wafuzu, wanatakiwa wapate matokeo bora kupita watakayopata Besiktas wanaocheza na CSKA Moscow.
Man U wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa Madifenda baada ya Wachezaji wao karibu wote wa pozisheni hizo kuumia.
Wachezaji hao ni Nemanja Vidic [mgonjwa wa mafua], Rio Ferdinand, John O'Shea, Jonny Evans, Gary Neville, Mapacha wa Brazil Rafael na Fabio, na Wes Brown.
Katika mechi hiyo ya leo Kiungo Michael Carrick anategemewa kucheza Sentahafu akishirikiana na Evra au Oliver Gill.
Meneja wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, amesema uteuzi wa Oliver Gill si upendeleo kwa sababu ni mwana wa Bosi bali ni kwa sababu ya uwezo wake.
Wadau wanahisi Timu ya Man U itakayocheza na Wolfsburg itakuwa: Kipa Foster, Walinzi: Park, Carrick, Fletcher, Evra.
Viungo: Scholes, Anderson, Gibson. Washambuliaji: Valencia, Owen, Obertan.
Fabregas "Arsenal inahitaji Straika!!"
Baada ya vipigo viwili mfululizo vya 3-0 mikononi mwa Manchester City kwenye Carling Cup na Chelsea kwenye Ligi Kuu, Nahodha wa Arsenal Cesc Fabregas amekiri kuwa Klabu yake inahitaji Sentafowadi mwenye miguvu kama Didier Drogba wa Chelsea.
Kwa sasa Arsenal wana upungufu wa Washambuliaji baada ya kuumia kwa Robin van Persie na Niklas Bendtner ambao watakuwa nje kwa muda mrefu huku Mafowadi wengine Eduardo na Rosicky huwa wanapata majeraha mara kwa mara.
Arsenal, mwanzoni mwa msimu, ilimuuza Sentafowadi hatari Emmanuel Adebayor kwa Manchester City.
Fabregas amebaini: "Katika mechi zote mbili tulizofungwa za Man City na Chelsea tulitawala na kumiliki mpira vizuri tu lakini umaliziaji ulikuwa duni, hatuna mtu tafu mbele! Chelsea ni Timu ya kawaida tu ila kwa kuwa wana Straika mwenye nguvu sana na bora, Drogba, wanashinda!"
Hata hivyo, kuna tetesi nzito kuwa dirisha la uhamisho likifunguliwa mwezi Januari Arsenal wataingia sokoni kumnunua Straika na Marouanne Chamakh kutoka Morocco anaechezea Klabu ya Bordeaux ndie mlengwa anaetajwa sana ingawa pia Mtaliana Mario Balotelli wa Inter Milan anatajwa pia.

Monday 7 December 2009

LIGI KUU England: Everton 2 Tottenham 2;
Fulham 1 Sunderland 0
Tottenham waliumwaga uongozi wa mabao 2-0 waliokuwa nao hadi dakika ya 78 na kuwaruhusu Everton kusawazisha na kuifanya mechi imalizike 2-2.
Ingawa Everton walisawazisha, Tottenham bado walikuwa na nafasi nzuri ya ushindi kwani walipewa penalti dakika za majeruhi lakini Jermaine Defoe alishindwa kufunga kwani mkwaju wake uliokolewa na Kipa Tim Howard.
Katika mechi hii ya Ligi Kuu iliyochezwa jana nyumbani kwa Everton Goodison Park, mechi ilikuwa 0-0 hadi mapumziko.
Dakika 2 baada ya kipindi cha pili kuanza Jermaine Defoe aliifungia bao Tottenham na Michael Dawson akaongeza bao la pili.
Everton walipata bao la kwanza kupitia Luis Saha dakika ya 78 na Tim Cahill akasawazisha.
Huko Craven Cottage nyumbani kwa Fulham, hapo jana wenyeji Fulham walipata bao moja na la ushindi kupitia Bobby Zamora dakika ya 7 na kuibwaga Sunderland kwenye mechi ya Ligi Kuu.
England yakana Wachezaji kupewa Viagra kwenye Fainali Kombe la Dunia!!!
FA, Chama cha Soka England, kimekana vikali taarifa zilizozagaa kuwa Wachezaji wa Kikosi cha England kwenye Fainali Kombe la Dunia mwakani huko Afrika Kusini watapewa dawa aina ya Viagra ili kumudu kucheza katika viwanja vilivyo juu sana toka usawa wa bahari ambako hewa ya oksijeni huwa pungufu na hivyo kufanya kupumua kuwe shida.
Inaaminika dawa ya Viagra, licha ya kuongeza nguvu za tendo la ndoa, pia humfanya mtu apumue vizuri hasa kwa Wanamichezo wanaoshindana kwenye viwanja vilivyo juu sana ambako kupumua kunakuwa shida.
Ripoti hizo za Wachezaji kupewa Viagra zilisema Kocha wa England Fabio Capello ndie alieamrisha kupewa dawa hizo lakini FA imekana taarifa hizo na kuziita za uzushi huku wakisistiza suala kucheza kwenye viwanja vya mwinuko wa juu linafanyiwa utafiti na Jopo lao la Madaktari ili kupata njia sahihi ya kukabiliana nalo.

Sunday 6 December 2009

Ancelotti: "Kipigo hakitubabaishi!"
Licha ya kubamizwa 2-1 na Manchester City hapo jana kwenye mechi ya LIGI KUU England, Meneja wa Chelsea Carlo Ancelotti amedai kipigo hicho hakiwasumbui kwani bado wanaongoza Ligi kwa pointi 2 mbele ya Timu ya pili Mabingwa Watetezi Manchester United.
Ancelotti amesema: "Kwa sasa tunafanya vizuri tu lakini jana ilikuwa ngumu kwani Man City walicheza vizuri mno!!"
Hata hivyo, Carlo Ancelotti alilamika kuhusu Refa Howard Webb kwa kulikubali goli la kusawazisha la Man City baada ya Mchezaji wa Man City Micah Richards kuunekana akiunawa mpira kabla ya Adebayor kufunga.
MSIMAMO LIGI KUU England:
1 Chelsea pointi 36
2 Man Utd pointi 34
3 Arsenal pointi 28
4 Tottenham pointi 26
5 Aston Villa pointi 26
6 Man City pointi 25
7 Liverpool pointi 24
8 Birmingham pointi 21
9 Sunderland pointi 20
10 Stoke pointi 20
11 Fulham pointi 19
12 Blackburn pointi 18
13 Burnley pointi 17
14 Wigan pointi 17
15 Hull pointi 16
16 Everton pointi 15
17 West Ham pointi 14
18 Wolverhampton pointi 13
19 Bolton pointi 12
20 Portsmouth pointi 10
RATIBA WIKI IJAYO:
UEFA CHAMPIONS LEAGUE
JUMANNE, 8 Desemba 2009
Atletico Madrid v FC Porto
Besiktas v CSKA Moscow
Chelsea v Apoel Nicosia
FC Zurich v AC Milan
Juventus v Bayern Munich
Maccabi Haifa v Bordeaux
Marseille v Real Madrid
Wolfsburg v Man Utd
JUMATANO, 9 Desemba 2009
Dynamo Kiev v Barcelona
Inter Milan v Rubin Kazan
Liverpool v Fiorentina
Lyon v Debrecen
Olympiakos v Arsenal
Sevilla v Rangers
Standard Liege v AZ Alkmaar
VfB Stuttgart v Unirea Urziceni
LIGI KUU ENGLAND:
JUMAMOSI, 12 Desemba 2009
Birmingham v West Ham
Bolton v Man City
Burnley v Fulham
Chelsea v Everton
Hull v Blackburn
Man Utd v Aston Villa
Stoke v Wigan
Sunderland v Portsmouth
Tottenham v Wolverhampton
JUMAPILI, 13 Desemba 2009
Liverpool v Arsenal
Defensi yote Man U majeruhi!!!
Meneja wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, hajui wapi atapata Madifenda kwa ajili ya mechi ya Jumanne huko Ujerumani dhidi ya Wolfsburg ambayo ni mechi ya mwisho ya Kundi lao ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE.
Sir Alex Ferguson amesema Walinzi wake Wanane ni majeruhi na ndio maana kwenye mechi ya jana ya LIGI KUU waliyocheza ugenini na kuifunga West Ham mabao 4-0 walimchezesha Kiungo wao Darren Fletcher kama Beki wa kulia na Garry Neville akacheza Sentahafu akishirikiana na Wes Brown huku Patrice Evra akicheza pozisheni yake ya kawaida Beki wa kushoto.
Defensi hiyo ilichezeshwa kwa sababu Madifenda Rio Ferdinand, Jonny Evans na John O’Shea ni majeruhi na Nemanja Vidic alikuwa akiugua flu.
Lakini baadaye kwenye mechi hiyo ya jana, Gary Neville na Wes Brown ilibidi watoke baada ya kuumia na ilibidi Michael Carrick, ambae kawaida ni Kiungo, acheze kama Sentahafu akishirikiana na Patrice Evra huku Ryan Giggs acheze kama Beki wa kushoto.
Ingawa Manchester United wameshafuzu kuingia Raundi inayofuata ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE, wanahitaji pointi 1 tu ili kujihakikishia wanabaki vinara wa Kundi lao na hivyo kukwepa kupangiwa Timu ngumu Raundi ijayo.
MATOKEO LIGI KUU England Mechi za Jumamosi Desemba 5:
Man City 2 Chelsea 1
Arsenal 2 Stoke 0
West Ham 0 Man U 4
Wigan 2 Birmingham 3
Blackburn 0 Liverpool 0
Aston Villa 3 Hull 0
Wolves 2 Bolton 1
Portsmouth 2 Burnley 0
MECHI ZA LEO DESEMBA 6 ZA LIGI KUU:
Fulham v Sunderland
Everton v Tottenham
Powered By Blogger