Sunday 6 December 2009

Defensi yote Man U majeruhi!!!
Meneja wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, hajui wapi atapata Madifenda kwa ajili ya mechi ya Jumanne huko Ujerumani dhidi ya Wolfsburg ambayo ni mechi ya mwisho ya Kundi lao ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE.
Sir Alex Ferguson amesema Walinzi wake Wanane ni majeruhi na ndio maana kwenye mechi ya jana ya LIGI KUU waliyocheza ugenini na kuifunga West Ham mabao 4-0 walimchezesha Kiungo wao Darren Fletcher kama Beki wa kulia na Garry Neville akacheza Sentahafu akishirikiana na Wes Brown huku Patrice Evra akicheza pozisheni yake ya kawaida Beki wa kushoto.
Defensi hiyo ilichezeshwa kwa sababu Madifenda Rio Ferdinand, Jonny Evans na John O’Shea ni majeruhi na Nemanja Vidic alikuwa akiugua flu.
Lakini baadaye kwenye mechi hiyo ya jana, Gary Neville na Wes Brown ilibidi watoke baada ya kuumia na ilibidi Michael Carrick, ambae kawaida ni Kiungo, acheze kama Sentahafu akishirikiana na Patrice Evra huku Ryan Giggs acheze kama Beki wa kushoto.
Ingawa Manchester United wameshafuzu kuingia Raundi inayofuata ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE, wanahitaji pointi 1 tu ili kujihakikishia wanabaki vinara wa Kundi lao na hivyo kukwepa kupangiwa Timu ngumu Raundi ijayo.
MATOKEO LIGI KUU England Mechi za Jumamosi Desemba 5:
Man City 2 Chelsea 1
Arsenal 2 Stoke 0
West Ham 0 Man U 4
Wigan 2 Birmingham 3
Blackburn 0 Liverpool 0
Aston Villa 3 Hull 0
Wolves 2 Bolton 1
Portsmouth 2 Burnley 0
MECHI ZA LEO DESEMBA 6 ZA LIGI KUU:
Fulham v Sunderland
Everton v Tottenham

No comments:

Powered By Blogger