Tuesday 8 December 2009

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: Real, Juve, AC Milan na Bayern kusonga leo?
Klabu vigogo huko Ulaya, Real Madrid, Juventus, AC Milan na Bayern Munich, ambao wote washawahi kuwa Mabingwa wa Ulaya, leo wanacheza mechi zao za mwisho za Makundi yao huku wote bado hawana uhakika wa kuingia Raundi inayofuata.
Rea Madrid, wanaocheza ugenini na Marseille, wana afueni kwani wanaweza kufungwa hata goli 3 na kusonga mbele wakati AC Milan lazima waifunge FC Zurich ili wasonge mbele.
Bayern Munich wanasafiri kwenda Italia kucheza na Juventus na lazima washinde huku Juve wakihitaji suluhu tu.
Klabu za England, Manchester United na Chelsea, tayari zishafuzu kuingia Raundi inayofuata na leo wanamaliza mechi zao kwenye Makundi yao, na ili wajihakikishie kuwa vinara wa Makundi hayo, wanahitaji angalau sare tu.
RATIBA MECHI ZA LEO Jumanne, 8 Desemba 2009
Atletico Madrid v FC Porto
Besiktas v CSKA Moscow
Chelsea v Apoel Nicosia
FC Zurich v AC Milan
Juventus v Bayern Munich
Maccabi Haifa v Bordeaux
Marseille v Real Madrid
Wolfsburg v Man Utd
UKOSEFU WA MADIFENDA MAN U: Kinda wa Bosi aingizwa Kikosini!!
Oliver Gill, umri miaka 19, ambae ni mtoto wa David Gill, Mkurugenzi Mtendaji wa Manchester United, amechukuliwa kwenye Kikosi cha Timu hiyo ambayo leo usiku ipo Ujerumani kupambana na Wolfsburg kwenye mechi ya mwisho ya Kundi lao kwenye mashindano ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE.
Man U washafuzu kuingia Raundi inayofuata lakini wanahitaji sare ili wajihakikishie uongozi wa Kundi lao na pengine kupata unafuu wa kupangiwa mpinazini dhaifu Raundi inayofuata.
Wolfsburg, ili wafuzu, wanatakiwa wapate matokeo bora kupita watakayopata Besiktas wanaocheza na CSKA Moscow.
Man U wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa Madifenda baada ya Wachezaji wao karibu wote wa pozisheni hizo kuumia.
Wachezaji hao ni Nemanja Vidic [mgonjwa wa mafua], Rio Ferdinand, John O'Shea, Jonny Evans, Gary Neville, Mapacha wa Brazil Rafael na Fabio, na Wes Brown.
Katika mechi hiyo ya leo Kiungo Michael Carrick anategemewa kucheza Sentahafu akishirikiana na Evra au Oliver Gill.
Meneja wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, amesema uteuzi wa Oliver Gill si upendeleo kwa sababu ni mwana wa Bosi bali ni kwa sababu ya uwezo wake.
Wadau wanahisi Timu ya Man U itakayocheza na Wolfsburg itakuwa: Kipa Foster, Walinzi: Park, Carrick, Fletcher, Evra.
Viungo: Scholes, Anderson, Gibson. Washambuliaji: Valencia, Owen, Obertan.
Fabregas "Arsenal inahitaji Straika!!"
Baada ya vipigo viwili mfululizo vya 3-0 mikononi mwa Manchester City kwenye Carling Cup na Chelsea kwenye Ligi Kuu, Nahodha wa Arsenal Cesc Fabregas amekiri kuwa Klabu yake inahitaji Sentafowadi mwenye miguvu kama Didier Drogba wa Chelsea.
Kwa sasa Arsenal wana upungufu wa Washambuliaji baada ya kuumia kwa Robin van Persie na Niklas Bendtner ambao watakuwa nje kwa muda mrefu huku Mafowadi wengine Eduardo na Rosicky huwa wanapata majeraha mara kwa mara.
Arsenal, mwanzoni mwa msimu, ilimuuza Sentafowadi hatari Emmanuel Adebayor kwa Manchester City.
Fabregas amebaini: "Katika mechi zote mbili tulizofungwa za Man City na Chelsea tulitawala na kumiliki mpira vizuri tu lakini umaliziaji ulikuwa duni, hatuna mtu tafu mbele! Chelsea ni Timu ya kawaida tu ila kwa kuwa wana Straika mwenye nguvu sana na bora, Drogba, wanashinda!"
Hata hivyo, kuna tetesi nzito kuwa dirisha la uhamisho likifunguliwa mwezi Januari Arsenal wataingia sokoni kumnunua Straika na Marouanne Chamakh kutoka Morocco anaechezea Klabu ya Bordeaux ndie mlengwa anaetajwa sana ingawa pia Mtaliana Mario Balotelli wa Inter Milan anatajwa pia.

No comments:

Powered By Blogger