Thursday 10 December 2009

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: Arsenal, Liverpool zafungwa, Barca, Inter zasonga!!
Timu za England, Arsenal na Liverpool, jana zilifungwa kwenye mechi zao za mwisho za UEFA CHAMPIONS LEAGUE.
Ingawa Arsenal alifungwa 1-0 na Olympiacos, ambayo kwa ushindi huo imejihakikishia kuingia Raundi ya Pili, Arsenal tayari waliwakuwa washafuzu kuingia Raundi hiyo ya Pili na pia kuwa kiongozi wa Kundi lao. Hivyo, katika mechi hiyo isiyokuwa na maana, Arsenal walichezesha Wachezaji makinda.
Liverpool, ambao tayari walikuwa washabwagwa nje ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE na kutupwa kwenye EUROPA LIGI kwa vile wamemaliza nafasi ya 3 kwenye KUNDI lao, walifungwa na Fiorentina uwanja wa Anfield mabao 2-1 na hivyo kuihakikishia Fiorentina uongozi Kundi E.
Mabingwa Watetezi Barcelona waliifunga Dynamo Kiev 2-1 na kufuzu kuingia Raundi ya Pili huku wenzao Kundini Inter Milan pia wakiungana nao baada ya kuichapa Rubin Kazan 2-0.
Droo ya kuamua Timu zipi zinakutana Raundi ya Pili itafanyika Desemba 18 na mechi za Raundi ya Pili zitakazochezwa kwa Mtoano, nyumbani na ugenini, zitachezwa Februari 2010.
TIMU ZILIZOFUZU KUINGIA RAUNDI YA PILI BAADA YA MECHI ZA JANA:
KUNDI E:
-Fiorentina
-Lyon
KUNDI F:
-Barcelona
-Inter Milan
KUNDI G:
-Sevilla
-Stuttgart
KUNDI H:
-Arsenal
-Olympiacos
MATOKEO KAMILI MECHI ZA JUMATANO, 9 Desemba 2009
Dynamo Kiev 1 v Barcelona 2
Inter Milan 2 v Rubin Kazan 0
Liverpool 1 v Fiorentina 2
Lyon 4 v Debrecen 0
Olympiakos 1 v Arsenal 0
Sevilla 1 v Rangers 0
Standard Liege 1 v AZ Alkmaar 1
VfB Stuttgart 3 v Unirea Urzicen 1
TIMU ZOTE ZILIZOFUZU KUINGIA RAUNDI YA PILI:
KUNDI A:
-Bordeaux
-Bayern Munich
KUNDI B:
-Man U
-CSKA Moscow
KUNDI C:
-Real Madrid
-AC Milan
KUNDI D:
-Chelsea
-FC Porto
KUNDI E:
-Fiorentina
-Lyon
KUNDI F:
-Barcelona
-Inter Milan
KUNDI G:
-Sevilla
-Stuttgart
KUNDI H:
-Arsenal
-Olympiacos
TIMU ZILIZOMALIZA NAFASI YA 3 KWENYE MAKUNDI NA HIVYO KUINGIZWA EUROPA LIGI:
-Juventus
-Wolfsburg
-Marseille
-Apoel Nicosia
-Liverpool
-Rubin Kazan
-Unirea Urziceni
-Standard Liege

No comments:

Powered By Blogger