Saturday 26 June 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

ZIGO LA AFRIKA KICHWANI GHANA: Sisi wote ni NYOTA NYEUSI!!!
Walikuwepo Wenyeji Afrika Kusini, maarufu Bafana Bafana, walikuwepo, Ivory Coast na kina Drogba, Cameroun na Eto’o, Nigeria na Algeria, lakini sasa imebaki ‘Nyota Nyeusi’ tu, Ghana, iliyobeba matumaini yote ya Afrika katika Fainali za Kombe la Dunia za kihistoria kwa vile kwa mara ya kwanza zinachezwa Afrika.
Leo, Jumamosi Juni 26, huko Uwanja wa Royal Bafokeng, Rustenburg Ghana inaivaa USA kwenye mechi ya Raundi ya Pili.
Ikiwa Ghana watashinda watakuwa wameifikia rekodi ya Cameroun ya Mwaka 1990 na Senegal 2002 ya Nchi ya Afrika kuweza kutinga Robo Fainali za Kombe la Dunia.
Ghana, bila Supastaa Michael Essien wa Chelsea, imewasuuza wengi akiwemo Jomo Sono wa Afrika Kusini ambae alikuwa maarufu kama Mchezaji na Mdau mkubwa wa Soka huko Bondeni na ambae ameisifia kwa kusema: “Ghana hawana majina makubwa, hawana wale Wachezaji nnaowaita wa Luninga! Wao wanacheza kitimu na kusaidiana. Hawana ubinafsi kama wengine!”
MUNGU IBARIKI GHANA, MUNGU IBARIKI AFRIKA!
AMINA.

No comments:

Powered By Blogger