Monday, 21 June 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

KOMBE LA DUNIA:
PATASHIKA KUINGIA RAUNDI YA PILI: Makundi A & B wacheza mechi za mwisho kesho Jumanne Juni 22
KUNDI A:
Msimamo:
-Uruguay pointi 4
-Mexico pointi 4
-France pointi 1
-South Africa pointi 1
Mechi za mwisho za Kundi hili ni Uruguay v Mexico na France v South Africa.
Uruguay na Mexico zinataka suluhu tu ili zitinge Raundi ya Pili na hilo limeleta minong’ono ya pengine Timu hizo zitafanya njama ya kuipata hiyo sare ili wote wasonge mbele.
Kwa Ufaransa na Bafana Bafana hamna njia ya mkato.
Ni lazima kila mmoja ashinde mechi yake na kisha aombe Mungu mechi ya Mexico v Uruguay imalizike kwa mmoja kufungwa.
Lakini hata maombi hayo pengine yasiwe yanatosha kwani vilevile ni lazima ushindi wa Ufaransa au Afrika Kusini uwe na magoli mazuri ili kuzipiku Mexico na Uruguay.
Ni kimbembe.
KUNDI B:
Msimamo:
-Argentina pointi 6
-South Korea pointi 3
-Nigeria pointi 1
-Greece pointi 1
Argentina tayari yuko Raundi ya Pili.
Kimbembe ni nani kati ya South Korea, Nigeria au Ugiriki ataungana na Argentina kutoka Kundi hili kwenda Raundi ya Pili.
Mechi za mwisho ni Argentina v Greece na Nigeria v South Korea.
Kwa Korea Kusini hata sare inaweza kuwasaidia ikiwa tu Ugiriki itatoka sare au kufungwa na Argentina.
Kwa kila hali, kwa South Korea, Nigeria na Ugiriki, ushindi ni kitu cha kwanza muhimu na mengine baadae.
Muntari aonywa na Ghana FA
Kiungo Sulley Muntari almanusura afungishwe virago toka huko Afrika Kusini ambako yuko na Ghana kwenye Kombe la Dunia lakini akapona kwa kupewa onyo kali na Chama cha Soka cha Ghana baada ya kukwaruzana na Kocha wa Ghana Milovan Rajevac anaetoka Serbia.
Muntari amekuwa hana rekodi nzuri na Timu ya Ghana na mara nyingi amekuwa akikwaruzana na Uongozi na visa kama hivyo vilimfanya asichukuliwe kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika huko Angola mapema Mwaka huu.
Ghana ndio wanaoongoza Kundi D na wanacheza mechi ya mwisho Jumatano na Ujerumani na sare tu itawatosha kutinga Raundi ya Pili ya Kombe la Dunia.

No comments:

Powered By Blogger