Thursday 24 June 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Beckenbaauer achochea uhasama England na Germany
Franz Beckenbauer ameiponda England na kuwaita wapumbavu kwa kushindwa kumaliza Kundi lao wakiwa vinara na hivyo kukwepa kucheza na Germany Raundi ya Pili ya Kombe la Dunia.
England walimaliza Kundi C wakiwa nafasi ya pili nyuma ya USA ambao watacheza na Ghana.
Beckenbauer, aliekuwa akiitwa ‘Der Kaiser’ enzi zaki akichezea Germany, amesema anaamini pambano la England v Germany halipaswi kuchezwa Raundi ya Pili na badala yake lingefaa kabisa kuwa Fainali.
Katika Fainali za Kombe la Dunia, England na Germany zimewahi kukutana mara 3 zikiwa ni Fainali Mwaka 1966 ambayo England waliifunga Germany 4-2 na kutwaa Ubingwa wa Dunia, na mara nyingine ni Robo Fainali Mwaka 1970 na Nusu Fainali Mwaka 1990.
Akizidi kutia utambi, Beckenbauer amesema Wachezaji wa England ni wachovu kwa kushindwa kuzifunga USA na Algeria.
Beckenbauer amesema: “Gemu ya England v Germany haifai kuwa ya Raundi ya Pili. Ni gemu kubwa sana na haisahauliki kwenye historia! Huu ni upumbavu wa England kwa kumaliza wa pili kwenye Kundi lao!”

No comments:

Powered By Blogger