Wednesday 23 June 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Man United yatoa nje kwa Cole
Manchester United wametangaza kuwa hawana nia ya kumchukua Joe Cole ambae sasa ni Mchezaji huru baada ya kumaliza Mkataba wake na Chelsea mwanzoni mwa Mwezi Juni.
Afisa wa ngazi za juu wa Man United amethibitisha kuwa hawana nia ya kumchukua Joe Cole, Miaka 28, ingawa kulikuwa na habari nyingi za kumhusisha na Old Trafford.
Klabu nyingine ambazo zinadaiwa zina nia ya kumchukua Cole ni Arsenal na Tottenham.
Cole kwa sasa yuko Afrika Kusini kwenye Kombe la Dunia pamoja na Kikosi cha England.
Cole alianza Soka lake huko West Ham kisha akahamia Chelsea Mwaka 2003 ambako amecheza mechi 396 na kuifungia Chelsea bao 52.
KOMBE LA DUNIA:
RATIBA-Alhamisi Juni 24
[saa za bongo]
Saa 11 jioni: KUNDI F
Paraguay v New Zealand Peter Mokaba, Polokwane
Slovokia v Italy Ellis Park, Johannesburg
Saa 3.30 usiku: KUNDI E
Denmark v Japan Royal Bafokeng, Rustenburg
Cameroun v Netherlands Green Point, Cape Town
Villa kupona rungu la FIFA
FIFA imethibitisha kuwa David Villa wa Spain hatachukuliwa hatua yeyote baada ya kunaswa na kamera akimpiga Beki wa Honduras Emilio Izaguirre tukio ambalo Refa toka Japan Yuichi Nishimura hakuliona.
Villa ndie alieifungia Spain bao zote mbili dhidi ya Honduras na pia alikosa penalti kwa kuipiga nje.
Msemaje wa FIFA amesema wamelichunguza tukio la Villa na hamna msingi wowote wa kufungua kesi.
Hivyo Villa yuko huru kucheza mechi ya mwisho ya Spain ya Kundi H watakapocheza na Chile ijumaa Juni 25.

No comments:

Powered By Blogger