Wednesday 25 November 2009

UEFA CHAMPIONS LEAGUE Leo:
FC Porto v Chelsea
Ingawa Klabu zote hizi mbili zimeshatinga Raundi nyingine ya mashindano haya, pambano hili la leo linalochezwa Estadio do Dragao huko Ureno lina umuhimu wa kuamua nani atamaliza yuko juu KUNDI D.
Chelsea wana pointi 10 toka mechi 4 na Porto wana 9.
Kocha wa Chelsea Catrlo Ancelotti amesema atawapumzisha Michael Essien na Didier Dogba ili wauguze maumivu yao na wawe fiti kwa mechi ya wikiendi ijayo ambapo Jumapili Chelsea watacheza na Arsenal kwenye Ligi Kuu.
Hata hivyo, Ancelotti amethibitisha kuwa Wachezaji wake wawili ambao ni Raia wa Ureno, Carvalho na Deco, watacheza mechi hiyo.
Man U v Besiktas
Manchester United tayari wameshaingia hatua inayofuata ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE na Sir Alex Ferguson ameshadokeza kuwa mechi hii ni sahihi kuwapa uzoefu Chipukizi wake kina Danny Welbeck, Obertan, Federico Macheda na Darren Gibson.
Pia, golini anaweza kuwepo Tomasz Kuszczak au Ben Foster ili kumpumzisha mkongwe Edwin van der Sar.
Kocha wa Besiktas, Mustafa Denizli, amekiri kuwa ni afadhali akutane na Timu kamili ya Man U kuliko Chipukizi wake kwa sababu wanawafahamu vizuri hao wakongwe na ni ngumu kuwakabili hao Chipukizi kwani hawawajui.

No comments:

Powered By Blogger