Monday 23 November 2009

GOLI 9 ZAMFEDHEHESHA KOCHA WIGAN!!!
Martinez: "Haikubaliki na hatukutegemea!"
Kocha wa Wigan, Roberto Martinez, amesema kipigo walichokipata jana Uwanjani White Hart Lane nyumbani kwa Tottenham ni fedheha na aibu kubwa.
Martinez amesema: "Ni fedheha! Tulilinda lango letu kijinga! Sijawahi kuhusika na gemu kama hii!"
Martinez ameendelea kusema walicheza vizuri hadi mapumziko huku Tottenham wakiongoza kwa bao la Peter Crouch lakini bao 5 za Jermaine Defoe kipindi cha pili ziliwaumiza.
Martinez ameongeza: "Tutachunguza kila kitu na kuangalia kila kitu! Inabidi tujue nini kilitokea na hilo litatufanya tuwe na nguvu baadae!"
Nae Meneja wa Tottenham, Harry Redknapp, amesema: "Ni siku mbaya kwa Martinez na ninamuheshimu sana!! Ni Meneja kijana mdogo mwenye kipaji na nina uhakika ataimarika zaidi na watalipiza kisasi kwa mtu!"

No comments:

Powered By Blogger