Sunday 22 November 2009

Tottenham 9 Wigan 1
Defoe afunga 5!!!
Mechi hii ya Ligi Kuu iliyochezwa leo huko White Hart Lane ilikuwa 1-0 mpaka haftaimu huku Tottenham wakiwa mbele kwa bao la Peter Crouch.
Lakini kipindi cha pili mambo yaligeuka na Mshambuliaji wa Tottenham Jermaine Defoe akacharuka na kufunga bao 5 na kumfanya aweke rekodi ya kuwa mmoja wa Wachezaji watatu waliowahi kufunga bao 5 katika mechi moja ya Ligi Kuu wengine wakiwa ni Alan Shearer wa Newcastle na Andy Cole wa Manchester United.
Na hii ni mara ya pili kwa Timu kuifunga Timu nyingine kwenye Ligi Kuu mabao 9 mara ya kwanza ikiwa ni mwaka 1995 pale Manchester United walipoibamiza Ipswich Town mabao 9-0.
Wafungaji wengine wa Tottenham mbali ya bao la kwanza la Crouch na 5 za Defoe ni Aaron Lennon, Niko Krancjar na Kipa wa Wigan Chris Kirkland kujifunga mwenyewe baada ya mpira kugonga posti na kumpiga mgongoni.
Bao la Wigan lilifungwa na Paul Scharner.

No comments:

Powered By Blogger