Tuesday 24 November 2009

Portsmouth wamtimua Meneja!!!
Klabu ya Portsmouth ambayo ndiyo inashika mkia kwenye msimamo wa Ligi Kuu England leo imemfukuza kazi Meneja wao Paul Hart.
Msimu huu, Portsmouth imecheza mechi 13 za Ligi Kuu na kushinda 2, kutoka sare 1 na kufungwa mechi 10.
Portsmouth imesema haikutaka kumfukuza Hart na ilitaka kumbadili kazi na kumpa posti ya Mkurugenzi wa Ufundi ili asimamie na kukuza vipaji vya Timu yao ya Vijana wa kati ya umri wa miaka 18 hadi 21 lakini Hart akagomea mabadiliko hayo.
Klabu hiyo imesema sasa Timu itakuwa chini ya Makocha wa Timu ya Kwanza Paul Groves na Ian Woan hadi hapo atakapopatikana mtu wa kudumu.
Portsmouth imekuwa ikikumbwa na matatizo ya kifedha na iliuzwa hivi karibuni lakini mnunuzi huyo nae akaiuza na mpaka sasa ina utata kwenye umilikwaji wake.

No comments:

Powered By Blogger