Wiki mbili Capello kujua hatma yake England!!
Kocha wa England Fabio Capello ametamka hatajiuzulu kufuatia kutolewa nje ya Kombe la Dunia kwa kipigo kitakatifu cha bao 4-1 toka kwa Germany hapo jana na pia ana nia kubwa ya kuendelea na kazi hiyo lakini amekiri kuwa itamchukua Wiki mbili kujua kama ataendelea kuwepo kwa vile FA bado inatafakari nini kifanywe.
Capello anao Mkataba na FA ambao utamalizika Mwaka 2012 mara tu baada ya Fainali za EURO 2012, michuano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya.Msemaji wa FA amesema hawawezi kutoa uamuzi mara tu baada ya kubwagwa nje ya Kombe la Dunia kwani hilo linaweza kuathiri kutoa uamuzi sahihi na badala yake kutoa uamuzi kwa jazba.
Mwenyewe Capello amesema: “Bado naitaka kazi hii ya England na ndio maana nimekataa kuwa Meneja wa Klabu kubwa kadhaa zinazonitaka.”
Capello aligusia sababu za England kuwa goigoi kwenye Kombe la Dunia na kudai sababu kubwa ni uchovu wa Wachezaji uliosababishwa na kutokuwa na mapumziko majira ya baridi [Desemba na Januari] kama wanavyofanya Nchi nyingine [ikiwemo Ujerumani] ambao Misimu yao huanza Agosti hadi mwishoni mwa Desemba na kupumzika na kisha kuanza tena mwishoni mwa Januari hadi Mei.
England Msimu huanza Agosti hadi Mei mfululizo bila mapumziko.
No comments:
Post a Comment