Monday 12 October 2009

FIFA U-20 WORLD CUP EGYPT 2009
Kesho Nusu Fainali!!
Mashindano ya Kombe la Dunia kwa Vijana wa Chini ya Miaka 20 yanayochezwa huko Misri kesho yapo Nusu Fainali na mechi zote mbili zitachezwa hiyo kesho kwa Brazil kukutana na Costa Rica na Ghana kucheza na Hungary.
Fainali ni Ijumaa tarehe 16 Oktoba 2009.
Hargreaves: Nipo imara!!
Mchezaji wa Manchester United Owen Hargreaves amsema hana wasiwasi na atarudi uwanjani, baada ya kuwa nje kwa zaidi ya mwaka mmoja alipokuwa akitibiwa magoti yake, akiwa bora na fiti zaidi.
Mechi ya mwisho Hargreaves kuichezea Klabu yake ilikuwa dhidi ya Chelsea miezi 13 iliyopita na baada ya hapo alipelekwa Marekani kufanyiwa upasuaji magoti yake yote mawili kwenye Kliniki ya Dr Richard Steadman ambae ni Mtaalam aliewatibu kina Tiger Woods, Alan Shearer, Michael Owen na Ruud van Nistelrooy magoti kwa kutumia upasuaji na matibabu ya kisasa kabisa.
Hargreaves amesema: “Nitajitahidi nipate mafanikio! Nataka nilipe fadhila kwa Mashabiki kwa kuwa na imani na mimi!”

Ben Foster aitwa Kikosi cha England, Rooney ajitoa!
Kocha wa England, Fabio Capello, amemwita Kipa wa Manchester United Ben Foster kwenye Kikosi cha England kitakachocheza mechi ya mwisho ya Kundi lao Uwanjani Wembley Jumatano na Belarus ili kuchukua nafasi ya Robert Green aliefungiwa mechi hiyo baada ya kupewa Kadi Nyekundu katika mechi na Ukraine Jumamosi iliopita ambayo England walifungwa 1-0.
Mechi haina umuhimu wowote kwa England ambao tayari wako Fainali Kombe la Dunia huko Afrika Kusini.
Ben Foster hakuchaguliwa kwenye Kikosi cha England kilichocheza na Ukraine na ilitolewa sababu kuwa alikuwa majeruhi ingawa dhana ya wengi ni fomu yake hasa baada ya kuifungisha Manchester United kwenye mechi za Ligi Kuu walizocheza na Manchester City na Sunderland.
Wakati huohuo, Straika Wayne Rooney amejitoa kwenye Kikosi cha England baada ya kuumia musuli ya mguu nyuma ya ugoko.
Heskey: Ntahama Villa ili niende Fainali Kombe la Dunia!!
Emile Heskey ametoboa kuwa ikifika Januari wakati dirisha la uhamisho litakapofunguliwa ataomba kuihama Klabu yake Aston Villa ikiwa hachezeshwi ili kwenda Klabu nyingine atayopata namba kwa sababu anataka kuweka hai nafasi yake kuichezea England Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwakani.
Jumamosi Emile Heskey alianza kwenye Kikosi cha England kilichofungwa na Ukraine 1-0 ikiwa ni mara yake ya 57 kuichezea England na ni mara ya 3 msimu huu kuichezea England lakini Klabuni kwake Aston Villa ameanza mechi moja tu msimu huu.
Aston Villa mara nyingi huwaanzisha Gabriel Agbonlahor na John Carew.
Heskey alihamia Aston Villa akitokea Wigan Januari mwaka huu.
MATOKEO KOMBE LA DUNIA:
Oktoba 11:
AFRIKA:
Benin 1 v Ghana 0
Nigeria 1 v Mozambique 0
Tunisia 1 v Kenya 0
Guinea 1 v Burkina Faso 2
Mali 1 v Sudan 0
Algeria 3 v Rwanda 1
MAREKANI YA KUSINI:
Bolivia 2 Brazil 1

No comments:

Powered By Blogger