Saturday 17 October 2009

Kama Fergie nae Wenger amkandya Refa Alan Wiley!!!
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, ameungana mkono na Sir Alex Ferguson wa Manchester United kwa kumlaumu Refa Alan Wiley lakini Wenger hakudai, kama alivyodai Ferguson, kuwa Refa huyo hayuko fiti ila amesema Refa huyo huongea vizuri sana na yuko karibu mno na Wachezaji.
Wenger anadai alimwona Refa Alan Wiley akiongea na Mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney, wakati wa haftaimu wa mechi moja na hilo limemkera Wenger ambae amesema: “Naamini Marefa ili wafanye kazi yao vyema ni lazima wasiwe na uhusiano na Wachezaji na Mameneja!”
Nae Mlinzi na Nahodha wa Manchester United, Gary Neville, amemtetea Meneja wake Sir Alex Ferguson katika mzozo kuhusu Refa Wiley alipomwita hayuko fiti kwa kusema: “Wamemwandama Meneja wetu lakini Refa Wiley alikuwa akitumia muda mrefu sana kuwaonya Wachezaji na kuwaandika kwenye kitabu chake! Wachezaji na Mameneja hawawezi kushinda! Mashabi na kadamnasi inataka ukweli lakini FA inatushitaki sisi Wachezaji na Mameneja tukisema ukweli!”
Sir Alex Ferguson ametakiwa na FA kutoa maelezo kuhusu kauli yake ya kuwa Refa Alan Wiley hayuko fiti na inategemewa wiki ijayo FA itaamua kumfungulia mashitaka au la.

No comments:

Powered By Blogger