Wednesday 7 July 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Ratiba ya Mechi za Ufunguzi Ligi Kuu England yapanguliwa!
Ili kukidhi mahitaji ya Stesheni za TV kurusha moja kwa moja matangazo ya mechi za Ligi Kuu, baadhi ya mechi za ufunguzi wa Msimu mpya wa 2010/11 zimebadilishwa Siku na saa.
Mechi ya kwanza kabisa ya Ligi Kuu itakuwa ni Jumamosi Agosti 14, saa 8 dakika 45 mchana kati ya Tottenham na Manchester City.
Mechi nyingine 6 Siku hiyo zitaanza saa 11 jioni na ya mwisho itakuwa saa 1 na nusu usiku wakati Mabingwa Chelsea watakapoanza kampeni ya kutetea Ubingwa wao kwa kuikaribisha Stamford Bridge Timu iliyopanda Daraja, West Bromwich Albion.
Jumapili, Agosti 15 kutakuwa na mechi moja tu nayo ni BIGI MECHI huko Anfield kati ya Liverpool na Arsenal itakayoanza saa 12 jioni na hii itakuwa ni mechi ya kwanza kwa Meneja mpya wa Liverpool Roy Hodgson alietokea Fulham.
Manchester United wataanza vita yao ya kulirudisha Taji Old Trafford kwa mechi hapo Old Trafford dhidi ya Timu iliyopanda Daraja Newcastle Siku ya Jumatatu Agosti 16 saa 4 usiku.
RATIBA KAMILI MECHI ZA UFUNGUZI:
[saa za bongo]
Jumamosi, 14 Agosti 2010
Tottenham v Man City, [saa 8.45 mchana]
[saa 11 jioni]
Aston Villa v West Ham,
Blackburn v Everton,
Blackpool v Wigan,
Bolton v Fulham,
Sunderland v Birmingham,
Wolverhampton v Stoke,
Chelsea v West Brom, [saa 1 na nusu usiku]
Jumapili, 15 Agosti 2010
Liverpool v Arsenal, [saa 12 jioni]
Jumatatu, 16 Agosti 2010
Man Utd v Newcastle, [saa 4 usiku]

No comments:

Powered By Blogger