Sunday, 4 July 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

KOMBE LA DUNIA:
Kimbembe cha NUSU FAINALI!!
Kwa ufupi tu........:
Holland v Uruguay
Jumanne saa 3.30 usiku [bongo]
Uwanja wa Green Park, Cape Town,
Historia fupi:
Uruguay ni Nchi ya Watu Milioni 3.5, imeshinda Kombe la Dunia mara mbili, Miaka ya 1930 na 1950, na kufika Nusu Fainali mara 3, Miaka ya 1954, 1970 na 2010.
Holland ni Nchi pekee Duniani kufika Fainali za Kombe la Dunia mara mbili mfululizo, Mwaka 1974 na 1978, na kufungwa mechi zote za mwisho na kuambulia ushindi wa pili.
Uholanzi imefikia hatua ya Nusu Fainali mara mbili Mwaka 1998 na 2010.
Mategemeo:
Kocha wa Holland, Bert van Marwijk, ametamka: “Furaha za huko nyumbani Uholanzi ni kubwa!”
Mashabiki 20,000 wa Holland walioko Cape Town wataomba nderemo ziendelee.
Kocha wa Uruguay, Oscar Tabarez, amenena: “Uholanzi ndio wanaotegemewa kushinda! Ni ngumu kwetu lakini sio kitu kisichowezekana!”
Ufunguo wa mechi:
Timu zote ni ngumu kwenye Difensi.
Uholanzi imefungwa bao 3 katika mechi 5 na Uruguay mbili tu.
Mechi hii itataka ubunifu wa Wachezaji Mastaa wa Timu huku Holland wakimtegemea Wesley Sneijder na Uruguay Diego Forlan kuifungua mechi hii.
Uteuzi wa Wachezaji:
Holland itamkosa Kiungo Mlinzi Nigel de Jong anaetumikia kifungo cha mechi moja na nafasi yake itachukuliwa na Stijn Schaars ingawa hata Rafael van der Vaart, kawaida ni Kiungo Mshambuliaji, anaweza kucheza.
Uruguay watamkosa Luis Suarez aliefungiwa mechi moja kwa kuleta ujangili mechi ya Ghana kwa kile alichokiita ‘Mkono wa Mungu’ na nafasi yake itazibwa na Sebastian Abreu.
Germany v Spain:
Jumanne saa 3.30 usiku [bongo]
Uwanja wa Moses Mabhida, Durban
Historia fupi:
Spain wana historia mbovu kwenye Kombe la Dunia.
Nafasi bora Spain waliyoweza kufika ni nafasi ya 4 Mwaka 1950 na hii ni mara ya kwanza kuingia Nusu Fainali.
Germany wao ni Mabingwa wa Dunia mara 3 na hii ni mara yao ya 12 kutinga Nusu Fainali.
Mategemeo:
David Villa, Mchezaji wa Spain anaeongoza kwa kupachika bao 5 kwenye Fainali hizi, anajipa matumaini: “Mpinzani kama Germany ndie anatupa changamoto kubwa na si Paraguay tulipocheza ovyo tu!”
Mashine ya Kijerumani ya Wachezaji Vijana zaidi wako watulivu bila mchecheto.
Ufunguo wa mechi:
Hii itakuwa mechi ambayo ushindi utapatikana kwa yule atakaetawala Kiungo.
Bila shaka, Xavi wa Spain na ile injini ya Ujerumani Bastian Schweinsteiger ndio watakaobeba Timu zao.
Uteuzi wa Wachezaji:
Kocha wa Ujerumani Joachim Low atalazimika kumbadilisha Thomas Muller na kumchezesha Piotr Trochowski kwa vile Muller amefungiwa mechi moja.
Spain wao, wakifanya badiliko lolote, itakuwa ni kimbinu tu kwani hawana majeruhi wala aliefungiwa na kuna minong’ono Fernando Torres, ambae kiwango kipo chini, huenda akabadilishwa na Llorente.

No comments:

Powered By Blogger