Webb wa England kuchezesha Fainali Kombe la Dunia

Refa Howard Webb atasaidiwa na wenzake toka England, Michael Mullarkey na Darren Cann.
Mpaka sasa huko Afrika Kusini, Webb na Timu yake wamechezesha Mechi 3, Spain walipofungwa 1-0 na Uswisi, Slovakia walipoibwaga Italy 3-2 na Brazil kuifunga Chile 3-0.
Katika mechi hizo tatu, Webb hakutoa Kadi Nyekundu wala penalti.
Webb na Wasaidizi wake ndio waliochezesha Fainali ya UEFA CHAMPIONS LIGI Mwezi Mei Inter Milan ilipoifunga Bayern Munich 2-0 huko Santiago Bernabeau na kutwaa Ubingwa wa Ulaya.
No comments:
Post a Comment