Tuesday 6 July 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Fergie: Zigo la kutegemewa limemwelemea Rooney!!!
Sir Alex Ferguson amedai kuwa Wayne Rooney alishindwa kung’ara kwenye Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini kwa sababu alielemewa na mzigo mzito wa kutegemewa na kila Mtu kuwa yeye ndie mkombozi wa England.
Ferguson, Meneja wa Manchester United, ambako Rooney aling’ara Msimu uliopita, amesema: “Nadhani matumaini makubwa ya kila Mtu yalimpa presha kubwa. Kila Mtu alidai Rooney ndie ataibeba England na atakuwa nyota kuliko Messi na Ronaldo. Watu wasubiri Fainali nyingine za Kombe la Dunia, baada ya Miaka minne Rooney ataibuka Mchezaji aliekomaa!”
Hata hivyo, Ferguson alionyeshwa kushangazwa na fomu ya England kwenye michuano hiyo ambayo walitolewa Raundi ya Pili walipopigwa 4-1 na Germany.
Lakini Ferguson amedai anaamini Germany wananufaika mno na kuwa na mapumziko ya Mwezi mmoja katikati ya Ligi yao Bundesliga ambayo huanza katikati ya Desemba hadi mwishoni Januari wakati ambao Ulaya hukumbwa na baridi kali.

No comments:

Powered By Blogger