MPIRA UTAKAODUNDA EURO 2008: ADIDAS 'EUROPASS'
Mpira utakaochezewa katika michuano ya EURO 2008 unaitwa ADIDAS “EUROPASS” na una rangi nyeupe na mabaka 12 meusi na nyongeza ya rangi ya fedha na nyekundu pamoja na bendera za Mataifa ya wenyeji wa mashindano Switzerland na Austria.
Mpira huu ambao umetengenezwa na Kampuni ya ADIDAS umeundwa kutoka vipande 14 kwa teknolojia ya kisasa kabisa. Mpira huu umepewa jina la “EUROPASS” kwa sababu mbili. Ya kwanza ni kumaanisha bonde la mpakani kati ya nchi hizi mbili wenyeji wa mashindano haya ya EURO 2008 yaani Switzerland na Austria.
Ya pili ni msisitizo wa pasi za uhakika za mpira katika mechi zenyewe.
Ngozi ya nje ya mpira huu imeundwa mahsusi na ina ‘vipele’ vidogo vitakavyosaidia usiteleze wakati unapopigwa au kudakwa na makipa huku ukichezeka vizuri tu katika hali zote za hewa iwe mvua, barafu au jua.
Majaribio ya mpira huu yalifanyika katika Chuo Kikuu cha Loughborough nchini Uingereza na katika Maabara Maalum ya Kampuni ya Adidas mjini Scheinfeld huko Ujerumani.
No comments:
Post a Comment