Friday 6 June 2008


Okocha aondolewa Hull City

Jay-Jay Okocha ametemwa na Hull City, timu mpya iliyopanda daraja kuingia LIGI KUU UINGEREZA, aliyojiunga nayo Septemba 2007 akitokea timu ya Qatar SC ya Qatar. Tangu alipojiunga na Hull City Okocha alicheza mechi 11 tu kwa kuwa majeruhi.
Hull City imepanda daraja kwenda LIGI KUU pamoja na timu za West Bromwich Albion na Stoke City.
Kabla ya kwenda Qatar, Okocha aliichezea Bolton Wanderers tangu Julai 2002 na alishiriki mechi 106 za LIGI KUU UINGEREZA na kufunga magoli 14 katika miaka minne aliyokuwa na timu hiyo.
Okocha alijiunga na Bolton akitokea Paris St Germain ya Ufaransa na ameichezea Timu ya Taifa ya Nigeria mara 70 na kushiriki katika Fainali za Kombe la Dunia mara tatu.

No comments:

Powered By Blogger