Friday 6 June 2008

Ronaldo avunja ukimya!
Winga wa Man U akubali anataka kujiunga Real ila kauli yake ni fumbo la utata!!

Tovuti ya Kibrazil iitwayo Terra imeripoti kumnukuu Ronaldo wakati akiwa kwenye kambi ya Timu yake ya Taifa ya Ureno huko nchini Uswisi mjini Neuchatel akijitayarisha kwa Fainali za EURO 2008 akisema: ‘Nataka kuchezea Real Madrid ikiwa tu ni kweli wako tayari kunilipa mimi na Manchester United kile wanachosema watalipa. Lakini, hii haitegemei kwangu. Ni muhimu kutuma ujumbe. Kuanzia sasa sizungumzi tena kuhusu hili mpaka mwisho wa EURO. Hamna faida kuniuliza swali kwani sitojibu.’

WADAU WAJITOSA KWENYE MJADALA:

Scotty Stevens (shabiki wa Manchester United) anasema...

Nakumbuka juzi tu Ronaldo katamka anataka kuwa staa wa MAN U kama kina George Best, Bobby Charlton, Cantona nk. Yeye kacheza miaka mitano tu na watu watamsahau! Moyoni namkumbuka sana na kumthamini sana Cantona aliechezea miaka minne na nusu tu na hakuwahi kuchukua Kombe la Ulaya!

John Clarke anena..

Kwaheri Ronaldo. Ulaghai wako wa kujiangushaangusha utapendwa sana huko Uhispania kwani ndio tabia yao! Ulafi na Pesa ndio mzizi wa mabaya yote duniani! Mie si mnazi wa ManU lakini nakubaliana na wote kwamba United ndio Klabu kubwa Ulaya na kuhama kwako ni kushuka ngazi. Nenda na potelea mbali!!

Thomas Vince (shabiki wa Arsenal) apasua...

Atakuwa mchezaji bora duniani akibaki Manchester United! Lakini huwezi kuwa na mchezaji asiekuwa na motisha na mapenzi klabuni kwako! Atafanya walichofanya Anelka na Thierry Henry na wengine wote waroho waliohamia Spain na wakadoda na hawakung’ara tena! Acheni ende na atajuta!. --

No comments:

Powered By Blogger