Wednesday 21 May 2008

DONDOO ZA FAINALI YA LEO KLABU BINGWA ULAYA






'FAINALI YA LEO ITAAMULIWA NA REFA!-ARSENE WENGER


Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, amejikita kwenye mjadala wa nani bingwa leo kati ya MAN U na CHELSEA huko LUZHNIKI STADIUM, MOSCOW, URUSI kwa kudai REFA, kutoka SLOVAKIA LUBOS MICHEL [pichani], ndie atakaeamua nani BINGWA. Kauli yake inafuatia madai yake kuwa msimu huu MAREFA walileta utata mkubwa.






REFA huyu wa leo tayari alishawaletea mzozo Chelsea mwaka 2005 alipowapa ushindi Liverpool katika nusu fainali ya mashindno haya aliporuhusu bao la Luis Garcia wakati Chelsea wnadai halikuvuka mstari.


===================================================



DROGBA: 'MAREFA HUNIONYA KABLA YA MECHI NISIJIANGUSHE MAKSUDI!'

Nyota wa Chelsea, Didier Drogba, amesema MAREFA wamekuwa na kawaida ya kumpa onyo kabla ya mechi kuwa asijifanye kuangushwa.

Nae anasema huwa nawajibu: 'MIE NI MWANASOKA NA SIO MWOGELEAJI!'

No comments:

Powered By Blogger