Saturday 24 May 2008

NANI ATAINGIA LIGI KUU: HULL CITY AU BRISTOL CITY?
fainali WEMBLEY leo saa 11 jioni!!

Mbele ya mashabiki wapatao 80,000 leo itapatikana timu ya tatu kupanda daraja kuungana na timu za WEST BROMWICH ALBION na STOKE CITY ambazo zilipanda kuingia LIGI KUU UINGEREZA moja kwa moja baada ya kushika nafasi za kwanza na za pili.
Timu zilizoingia fainali ya mtoano ya kupata timu ya tatu kupanda daraja ni timu za HULL CITY na BRISTOL CITY. Timu zote hizi hazijawahi kuchezea LIGI KUU.
HULL CITY iliitoa WATFORD kwa jumla ya mabao 6-1 na BRISTOL CITY iliifunga CRYSTAL PALACE jumla ya mabao 4-2.
Itakumbukwa timu zilizoshuka daraja ni DERBY, BIRMINGHAM na READING.

No comments:

Powered By Blogger