Tuesday 1 September 2009

Croatia wadai wanafanyiwa njama na England!!!
Croatia ambao wako Kundi moja pamoja na England kwenye mtoano wa kuingia Fainali ya Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwakani wametoa madai ya kushangaza sana waliposema kuwa kuna njama za kuwaumiza Wachezaji wao muhimu.
Mwaka jana Mchezaji wa Croatia Eduardo anaecheza Arsenal alivunjwa mguu na Mchezaji wa Birmingham Martin Taylor na alikaa nje ya uwanja mwaka mzima na kukosa kucheza EURO 2008 na Jumamosi iliyopita Mchezaji mwingine wa Croatia, Luka Modric, anaecheza Tottenham alivunjwa mguu na ni Mchezaji mwingine wa Birmingham, Lee Bowyer, aliemwumiza.
Jumatano ijayo Croatia inapambana na England Uwanjani Wembley katika Kombe la Dunia na England wakishinda watatinga Fainali huko Afrika Kusini.
Rais wa Chama cha Mpira cha Croatia, Vlatko Markovic, amechochea dhana ya njama kwa kutamka: “Pengine kuna mtu hatutakii mema!! Katika mwaka mmoja, England wamewaumiza nyota wetu wawili! Ni makusudi au bahati mbaya, hatujui!! Lakini, inashangaza haya matukio jinsi yanavyofanana!!”
Nae Mmiliki wa Birmigham, David Gold, amecheka alipoambiwa tuhuma za Croatia kwamba Klabu yake imeshiriki njama za England.
Gold alisema: “Kutuhusisha na kudai ni njama ni upumbavu wa hali ya juu!! Hivi kuna mtu anaamini tuhuma hizi? Sidhani!! Nadhani pengine hiyo taarifa toka Croatio imetafsiriwa vibaya!! Ni ngumu kuamini hili!!”

No comments:

Powered By Blogger