Tuesday 1 September 2009

Benitez mahakamani FA!!
Meneja wa Liverpool, Rafael Benitez, amefunguliwa mashtaka na FA, Chama cha Soka England, baada ya kukasirishwa na Refa Phil Dowd kuwanyima penalti 2 kwenye mechi ya Ligi Kuu walipofungwa 2-1 na Tottenham.
Benitez alimponda Mwamuzi wa Akiba Stuart Attwell, umri miaka 26, na kumwita bado mtoto mdogo kusimamia mechi ya Ligi Kuu mara baada ya Refa, baada ya kubonyezwa na Attwell, kuamuru Msaidizi wake Benitez, Sammy Lee, atolewa nje kwa kutumia lugha chafu.
Baada ya mechi hiyo, Benitez, akihojiwa na Waandishi alitamka kuwa ni vigumu kwa Refa huyo kutoa penalti kwao na kisha akatoa mawani yake mfukoni na kuyaonyesha akiashiria Refa Phil Dowd ni kipofu.
Kurasa 19 utetezi wa Eduardo UEFA!!
Arsenal imewasilisha kurasa 19 kwa UEFA ikiwa ni utetezi wa Mchezaji wao Eduardo alieshitakiwa kwa kosa la kumdanganya Refa Manuel Gonzalez na kupata penalti aliyoifungia Arsenal bao la kwanza kwenye mechi na Celtic ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE ambayo Arsenal alishinda 3-1.
Moja ya utetezi wa Arsenal ni kuwa baada ya kuichunguza video waliyoletewa na UEFA wamegundua kuwa Eduardo na Kipa wa Celitic Artur Boruc waligusana kidogo.
Arsenal vilevile wanadai mara baada ya Eduardo kudondoka hakudai faulo na ni Refa mwenyewe alietoa uamuzi huo. Pia, Arsenal wamesema baada ya Eduardo kuumizwa vibaya mwaka jana alipovunjwa mguu mara nyingi huwa anakwepa kugonganga na mtu uwanjani na ndio maana akaanguka.

No comments:

Powered By Blogger