Wednesday 2 September 2009

Arsenal yafadhaishwa kufungiwa Eduardo!!!
Kifungo cha Eduardo cha mechi mbili alichotwangwa na UEFA kimewakera na kuwafadhaisha Arsenal ambao sasa wanatafakari hatua gani wachukue.
Arsenal wamepewa siku 3 kukata rufaa.
Taarifa kwenye tovuti ya Arsenal imesema: “Klabu imevunjika moyo na uamuzi wa UEFA kumfungia Eduardo mechi 2 za UEFA CHAMPIONS LEAGUE ikianzia ile na Standard Liege tarehe 16 Septemba. Tumeambiwa mpaka Alhamisi tutapewa maelezo kamili kuhusu kesi ya Eduardo na mara tukiipata tutatoa uamuzi nini kitafuatia.”
Anelka achukizwa na Chelsea!!
Mshambuliaji wa Chelsea, Nicolas Anelka, inasemekana amekasirishwa sana na hatua ya Klabu yake kutompa mkataba mpya msimu huu.
Imebainika kuwa Anelka, umri miaka 30, ameambiwa kuwa msimamo wa Chelsea ni kutowapa Wachezaji wenye umri wa miaka 30 kwenda juu mikataba mipya hadi wanapoingia mwaka wao wa mwisho wa mkataba wao wa sasa.
Hatua hiyo ya Chelsea imemkasirisha sana Anelka anaehisi hathaminiwi hasa baada ya kuchelewesha kufanyiwa operesheni kutibu paja na nyonga kwa manufaa ya Klabu ili kumjengea mazingara mazuri Kocha mpya Carlo Ancelotti.
Hasira za Anelka zimezidishwa hasa baada ya Chelsea kuwapa Nahodha John Terry na Ashley Cole mikataba mipya.

No comments:

Powered By Blogger