Monday 16 June 2008


Siku mbaya kwa Brazil, Argentina katika michuano ya awali kuwania nafasi kuingia FAINALI KOMBE LA DUNIA 2010!
Timu ya Taifa ya Brazil ilifungwa 2-0 nchini Paraguay waliocheza watu 10 tu baada ya mlinzi wao kutolewa dakika ya 48 ya mchezo wakati Argentina pia ikicheza ugenini ilihitaji dakika za majeruhi kufunga bao la kusawazisha na kuambua sare ya 1-1 na Ecuador.
Mechi hizi ni za kundi la nchi 10 za Marekani ya Kusini zinazowania nafasi nne za kuingia FAINALI KOMBE LA DUNIA 2010 nchini AFRIKA KUSINI.
Baada ya mechi tano tano, Paraguay inaongoza ikiwa na pointi 13, Argentina inafuatia ikiwa na 10, Colombia 9, Brazil 8, Venezuela na Chile 7, Uruguay 5.
Hekaheka ni Jumatano wakati watani wa jadi Brazil watakapo wakaribisha Argentina.

No comments:

Powered By Blogger