Friday 20 June 2008

McClaren awa Meneja FC Twente
Meneja wa zamani wa Timu ya Taifa ya Uingereza Steve McClaren amerudi tena dimbani baada ya kupata kazi ya kuwa Meneja mpya wa Klabu ya Uholanzi FC Twente.
Klabu hiyo ipo daraja la juu la ligi za Uholanzi na itacheza mashindano ya LIGI YA KLABU BINGWA ULAYA msimu unaokuja na hilo ndio jukumu kubwa la kwanza la Steve McClaren.
McClaren aliiacha kazi ya Umeneja wa Uingereza Novemba mwaka jana mara tu baada ya Uingereza kukosa nafasi ya kucheza Fainali za EURO 2008. Kabla ya hapo alikuwa Meneja wa Middlesborough timu iliyoko LIGI KUU UINGEREZA na Meneja Msaidiza Man U chini ya Sir Alex Ferguson.

No comments:

Powered By Blogger