Saturday 21 June 2008





KUTOKA LIGI KUU UINGEREZA




  • MNIGERIA Julius Aghahowa amehama WIGAN na kusaini mkataba wa miaka mitatu na Klabu ya Uturuki Kayserispor. Aghahowa, miaka 26, anaondoka Wigan baada ya kukaa miezi 18 tu akitokea Klabu ya Urusi Shakhtar Donertsk. Akiwa na Wigan alicheza mechi 23 tu.
  • Mlinzi wa Arsenal Gael Clichy amesaini 'mkataba wa muda mrefu' Arsenal imetamka. Clichy, miaka 22, alitokea Klabu ya Ufaransa, Cannes mwaka 2003 na amejikita kwenye timu ya kwanza ya Arsenal baada ya beki Ashley Cole kuhamia Chelsea. Mpaka sasa, Clichy ameshacheza mechi 146 akiwa na Arsenal.
  • Paul Ince, miaka 40, aliekuwa kiungo mahiri wa Timu ya Taifa ya Uingereza na Klabu za West Ham, Man U, Inter Milan na Liverpool, anategemewa muda wowote kutangazwa kuwa Meneja mpya wa Klabu ya Blackburn Rovers ambayo kwa sasa haina Meneja baada ya Mark Hughes kuhamia Manchester City. Habari hizi zimepata nguvu hasa baada ya uongozi wa LIGI KUU kuwapa Blackburn Rovers kibali maalum kumtumia Paul Ince bila ya yeye kuwa na LESENI YA UKOCHA YA UEFA PRO. Leseni hii inahitajika kwa Mameneja wote wa ligi za juu za nchi nyingi Ulaya na ili kupata leseni hii inabidi upate masomo maalum ya zaidi ya masaa 240 na kawaida huchukua mwaka mmoja kuhitimu. Ince amepewa kibali hicho maalum cha miaka miwili. Ince kwa sasa ni Meneja wa MK Dons timu inayocheza daraja la chini LIGI YA PILI. Endapo Paul Ince atatangazwa kuwa Meneja wa Blackburn Rovers basi ataweka historia ya kuwa Meneja wa kwanza 'mweusi' wa Klabu ichezayo LIGI KUU UINGEREZA.




No comments:

Powered By Blogger