Saturday 21 June 2008






MECHI YA LEO ROBO FAINALI:
UHOLANZI v URUSI




Ni pambano la Mataifa mawili lakini ukweli ni kwamba ni mechi kati ya Waholanzi wawili!
Hiki ni kivutio maalum kwa mechi ya leo!
Marco van Basten, Mholanzi, ni Meneja wa Uholanzi, na Guus Hiddink ni Mholanzi pia lakini kwa sasa ni Meneja wa Urusi!
Mholanzi mmoja, Marco van Basten, aliweka historia ya kuwa mmoja wa 'mastaa' wakubwa katika historia ya soka ya wachezaji wa Uholanzi wakiwemo kina Johan Cruyff na mwingine ni Mholanzi, Guus Hiddink, aliyeleta mafanikio makubwa kwa nchi yake kwa kuiongoza kama Meneja na kumudu kuifikisha Nusu Fainali ya Kombe la Dunia 2008!
'Nina furaha kwa Guus,' alisema Marco van Basten.'Baada ya mwanzo mbaya kwenye EURO 2008 ameweza kuigeuza Urusi na kumfunga Sweden. Lakini timu yake inapambana na timu yangu yenye vipaji na uwezo mkubwa!'
Nae Guus Hiddink alinena:'Itakuwa ni mechi spesho kwangu. Namjua kila mtu kwenye kambi ile. Na kitu kinachonipa furaha zaidi ni kuona timu mbili zinazocheza kandanda safi zinakutana! Je tunaweza kuwafunga? Kwa nini isiwezekane? Lengo letu Urusi lilikuwa ni kufika Robo Fainali na tumetimiza lakini tutajitahidi zaidi.'


No comments:

Powered By Blogger