Monday 8 June 2009

WEST HAM YAPIGWA BEI!!!
Klabu ya LIGI KUU England West Ham imeuzwa na kununuliwa na Kampuni iitwayo CB Holdings ambayo ni Kampuni inayomilikiwa na Mabenki kadhaa ya Rasilimali toka Nchini Iceland.
Awali West Ham ilikuwa ni mali ya Raia wa Iceland aitwae Bjorgolfur Gudmundsson ambae mporomoko wa soko la fedha duniani umemuathiri sana na kumfanya ashindwe kuiendesha vizuri Klabu hiyo.
Kampuni ya CB Holdings imeahidi kumpa Meneja wa West Ham Giafranco Zola fedha za kununua Wachezaji wapya kwa msimu ujao na pia imeahidi kutoingilia uendeshwaji wa Klabu hiyo
MMILIKI WA NEWCASTLE ATAIUZA KLABU KWA PAUNI MILIONI 100!!
Mmiliki wa Newcastle Mike Ashley, Klabu iliyoporomoka Daraja kutoka LIGI KUU England, amethibitisha Klabu hiyo inauzwa kwa dau la Pauni Milioni 100 ikiwa ni thamani ndogo sana kuliko dau alilotoa kuinunua na kuwekeza kwenye Klabu hiyo.
Mpaka sasa Mike Ashley hajapata ofa thabiti ingawa Benki ya Rasilimali iitwayo Seymour Pierce imetamka vipo vikundi viwili vitatu vilivyoonyesha nia ya kuinunua.
Mike Ashley amekuwa kwenye mfarakano mkubwa tangu Meneja kipenzi wa Washabiki wa Newcastle ambae pia aliwahi kuwa Mchezaji nyota wa Klabu hiyo hapo zamani, Kevin Keagan, kubwaga manyanga mwaka jana mwanzoni mwa msimu uliokwisha mwezi Mei mwaka huu.
RATIBA KOMBE LA DUNIA:
ULAYA:
Jumatano, 10 Juni 2009
England v Andorra,
Faroe Islands v Serbia,
Finland v Russia,
FYR Macedonia v Iceland,
Netherlands v Norway,
Sweden v Malta,
Ukraine v Kazakhstan,
MAREKANI KUSINI:
Jumatano, 10 Juni 2009
Ecuador v Argentina
Colombia v Peru
Venezuela v Uruguay
Chile v Bolivia
Brazil v Paraguay

No comments:

Powered By Blogger