Tuesday 9 June 2009

Rais Zuma apokea Kombe la Mabara!!!
Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, leo amekabidhiwa Kombe la Mabara La FIFA na Katibu Mkuu wa FIFA Jerome Valckle, ikiwa heshima na utambulisho maalum kwa Mashindano yatakayoanza Jumapili Juni 14 yakiwa kama 'Fungua Pazia' kwa Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2010 ambayo Afrika Kusini ni wenyeji.
Rais wa Afrika Kusini, Mheshimiwa Zuma, akilipokea Kombe hilo, alitamka: 'Hii ni ishara muhimu 2010 imefika! Kikombe kiko hapa!'
Na ili kuipa Timu yake morali, Zuma akatamka kuwa Bafana Bafana wataweka historia kwa kulinyakua Kombe la Mabara na kwa kuweka msisitizo, mbele ya video na kamera zilizolipulika kila mara, akaonyesha utaalam wa kucheza na mpira aliopewa zawadi na Katibu Mkuu wa FIFA, Jerome Valckle.
Kombe la Mabara litaanza Jumapili Juni 14 na litawahusisha Wenyeji Afrika Kusini, Mabingwa wa Dunia Italia, Mabingwa Watetezi wa Kombe hilo Brazil, ambao pia ni Mabingwa wa Marekani ya Kusini, Spain, Egypt, New Zealand, Iraq na USA.

No comments:

Powered By Blogger