Friday 12 June 2009

Fabregas asisitiza yeye ni Arsenal!!
Cesc Fabregas, Nahodha wa Arsenal, ametoka hadharani kuzima minong’ono ya kila mara kwamba atarudi kwao Spain kujiunga na Barcelona Timu aliyoanza kuichezea akiwa mtoto.
Fabregas,22, ametamka: ‘Nina mkataba wa muda mrefu Arsenal na hapa nitabaki muda mrefu!’
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, alimpa Ukepteni Fabregas mwezi Novemba mwaka jana baada ya William Gallas kuvuliwa madaraka hayo.
Mkataba wa Fabregas utaisha 2014.
Deco anaitaka Inter!!!
Deco amesema hana furaha kuchezea Chelsea na anataka kwenda Italia akacheze Inter Milan kwa Kocha Mreno mwenzake Jose Mourinho ambae walikuwa nae pamoja Klabu ya FC Porto ya Ureno.
Baada ya FC Porto, Mourinho akaenda Chelsea na Deco akahamia Barcelona.
Deco, akitokea Barcelona, aliletwa Chelsea na Scolari aliekuwa Meneja wa Timu ya Taifa ya Ureno, baada ya Scolari kuingia Chelsea.
Tangu Scolari atimuliwe, Deco amekuwa hana namba.
Deco anaelezea kuhusu Mourinho: ‘Nataka niwe na Mourinho. Yeye ndio amesaidia mafanikio yangu.’

No comments:

Powered By Blogger