Thursday, 11 June 2009

WACHEZAJI England wa Kombe la Dunia mwaka 1966 hatimaye wapewa MEDALI ZAO!!
England iliwafunga Ujerumani Magharibi- wakati huo kulikuwa na Ujerumani mbili, Magharibi na Mashariki-mabao 4-2 mwaka 1966 Uwanjani Wembley na kutwaa Kombe la Dunia lakini ni Wachezaji 11 tu waliocheza mechi ile ndio walipewa Medali za Dhahabu kwa ushindi huo.

Huo ndio ulikuwa mtindo wa zamani kwamba ni yule tu alie kiwanjani ndie anaambua Medali na si Kikosi kizima.
Lakini FIFA imeamua hivi karibuni kuwapa Medali Wachezaji wote waliokuwa kwenye Kikosi cha Nchi iliyochukua Kombe la Dunia pamoja na Makocha na Wasaidizi wote kuanzia Fainali za mwaka 1930 hadi 1974.
Kuanzia Fainali za 1978 FIFA ilibadilisha mtindo na ikawa inatoa Medali kwa Kikosi kizima pamoja na Wasaidizi wa Timu.
Jana Wachezaji wa England wa Kikosi kilichochukua Kombe la Dunia mwaka 1966 ambao walikosa Medali walikabidhiwa Medali zao kwa niaba ya FIFA na Waziri Mkuu wa Uingereza Gordon Brown.
Wachezaji waliopewa Medali jana na kuzipokea wenyewe au Familia zao ni Peter Bonetti, Ron Springett, Jimmy Armfield, Gerry Byrne, Ron Flowers, Norman Hunter, Terry Paine, Ian Callaghan, John Connelly, George Eastham na Jimmy Greaves.
Baadae Wachezaji hao wa zamani na Familia zao walikuwa ndio wageni rasmi kwenye mechi ya mchujo wa Kombe la Dunia kati ya England na Andorra Uwanjani Wembley, jijini London ambayo England walishinda 6-0.
Pichani ni Jimmy Greaves na Norman Hunter wakifurahia Medali zao.

No comments:

Powered By Blogger