Saturday 21 November 2009

Roy Keane aiponda Nchi yake Ireland kwa kudai mechi na Ufaransa irudiwe
Nahodha wa zamani wa Manchester United na Mchezaji wa zamani wa Republic of Ireland, Roy Keane, ambae sasa ni Meneja wa Ipswich, amekilaumu FAI, Chama cha Soka Ireland, kwa kudai mechi kati ya Ufaransa na Ireland irudiwe baada ya Thierry Henry kuucheza kwa mkono mpira na kumpasia William Gallas aliefunga bao lililowapa Ufaransa sare 1-1 na hivyo ushindi wa jumla ya mabao 2-1 katika mechi mbili na kutinga Fainali Kombe la Dunia.
FAI imeiandikia barua FIFA kutaka mechi hiyo irudiwe lakini Roy Keane, ambae mwaka 2002 aliondoka kwa hasira kwenye Kikosi cha Ireland kilichokuwa Fainali za Kombe la Dunia huko Korea na Japan, amewalaumu sana Ireland na kuwataka wasilete madai ya kurudiwa mechi kwa sababu wao pia hawajui haki ni nini.
Keane ametamka: “Watalalamika mpaka watachoka, Ufaransa inaenda Fainali! Wasahau hilo!”
Akizungumzia kitendo cha Thierry Henry kuucheza mpira kwa mkono, Keane hakumlaumu Henry na badala yake aliilaumu Ireland.
Keane alisema: “Kwa nini defensi haikuundoa mpira? Kipa alikuwa wapi mpira ukiingia boksi la yadi 6? Kwa nini waruhusu mpira udunde kwenye hilo boksi?”
Rio kurudi baada ya wiki chache!!
Sir Alex Ferguson amesema wamegundua tatizo linalomkabili Sentahafu wao Rio Ferdinand na sasa anapewa tiba sahihi na atarudi uwanjani baada ya wiki chache na sio miezi kama inavyodiwa.
Ferdinand hajacheza wiki kadhaa sasa na Ferguson amesema tatizo lake ni mgongo sehemu za kiuno na hilo husabbabisha maumivu kwenye musuli za miguu.
Mwaka wote huu, Ferdinad amekuwa hachezi mara kwa mara kwa kuwa na maumivu.
Wakati Ferdinand yuko nje, Sentahafu mwingine Nemanja Vidic amepona na leo anategemewa kuanza mechi ya Ligi Kuu na Everton huko Old Trafford.

No comments:

Powered By Blogger