Thursday, 19 November 2009

LIGI KUU England kilingeni Jumamosi!
Fergie kuwepo benchi mechi ya Jumamosi na Everton!!
Baada ya karibu wiki 2 kutochezwa ili kupisha patashika ya mechi za Kombe la Dunia, Ligi Kuu England itarudi kwa kishindo kuanzia Jumamosi kwa kuchezwa mechi 7, Jumapili mechi 3 na Jumatano ijayo mechi 2.
Ingawa ilitegemewa Kocha wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, angeanza kutumikia kifungo chake cha mechi 2 Jumamosi hii kwa kutoruhisiwa kukaa benchi la Akiba la Timu yake katika mechi na Everton huko Old Trafford, FA imefafanua kuwa adhabu hiyo inaanza siku 14 tangu hukumu na hivyo Ferguson atakuwepo benchi Jumamosi na kuzikosa mechi za tarehe 28 Novemba watakapokuwa ugenini Portsmouth na ile ya Kombe la Carling na Tottenham tarehe 1 Desemba.
Ferguson atakuwa kifungoni baada ya kutiwa hatiani kwa kauli yake kwamba Refa Alan Wiley hayuko fiti kuchezesha mechi aliyoitoa Oktoba 3 mara baada ya sare ya Ligi Kuu ya 2-2 na Sunderland.
Mpaka sasa, baada ya mechi 12 kwa kila Timu, isipokuwa Arsenal na Manchester City zilizocheza 11, msimamo ni:
1. Chelsea pointi 30
2. Arsenal pointi 25
3. Man U pointi 25
4. Tottenham pointi 22
5. Aston Villa pointi 21
6. Man City pointi 20
7. Liverpool pointi 19
RATIBA:
Jumamosi, 21 Novemba 2009
Birmingham v Fulham
Burnley v Aston Villa
Chelsea v Wolves
Hull City v West Ham
Liverpool v Man City
Man U V Everton
Sunderland v Arsenal
Jumapili, 22 Novemba 2009
Bolton v Blackburn
Stoke v Portsmouth
Tottenham v Wigan
Jumatano, 25 Novemba 2009
Fulham v Blackburn
Hull City v Everton

No comments:

Powered By Blogger