Leo huko Abuja, Wenyeji Nigeria watavaana na Uswisi katika Fainali ya Kombe la Dunia la Vijana Chini ya Miaka 17.
Mechi hii itaanza saa 3 usiku saa za bongo.
Fainali hiyo itatanguliwa na Timu zilizobwagwa Nusu Fainali, Colombia v Spain, zitakazocheza kupata Mshindi wa 3.
Huko Ulaya KOMBE LA DUNIA: Ureno, Ufaransa na Urusi zaanza vyema mechi za Mtoano!!
MATOKEO MECHI ZA KWANZA ULAYA:
Ureno 1 Bosnia-Herzegovina 0
Urusi 2 Slovenia 1
Republic of Ireland 0 Ufaransa 1
Ugiriki 0 Ukraine 0
Ugiriki 0 Ukraine 0
Ureno, wakicheza nyumbani, waliifunga Bosnia-Herzegovina kwa bao lililofungwa na Bruno Alves.
Timu hizi zitarudiana Jumatano ili kupata Mshindi atakaetinga Fainali Kombe la Dunia Afrika Kusini mwakani.
Nao, Urusi wakicheza nyumbani waliipiga Slovenia 2-1 huku Mchezaji wa Everton, Diniyar Bilyaletdinov akiifungia bao zote mbili.
Timu hizi zitarudiana huko Slovenia Jumatano Novemba 18.
Na huko Dublin, Republic of Ireland ilfungwa ikiwa nyumbani na Ufaransa baada ya shuti la Nicolas Anelka kumbabatiza beki na kutinga wavuni.
Mechi ya mwisho kwa Nchi za Ulaya zinazocheza Mtoano ilikuwa ni kati ya Ugiriki na Ukraine na ngoma ikaisha 0-0 na marudio ni huko Ukraine Jumatano ijayo.
kombe la Dunia MATOKEO MECHI YA KWANZA MAREKANI:
Costa Rica 0 Uruguay 1
Katika mechi ya kwanza ya Mtoano huko Marekani, Uruguay ilipata bahati kubwa kwa kushinda ugenini kwa bao la Diego Lugano dakika ya 23.
Timu hizi zitarudiana huko Uruguay Jumatano Novemba 18.
MECHI YA KIRAFIKI: Doha, Qatar:
Brazil 1 England 0
Katika mechi ya kirafiki iliyochezwa Uwanja wa Khalifa mjini Doha, Qatar, Brazil iliishinda England kwa bao 1-0 kwa bao lililofungwa na Nilmar dakika ya 47.
Brazil walikosa penalti kwenye dakika ya 55 baada ya Luis Fabiano kupaisha shuti lake.
England iliyoongozwa na Nahodha Wayne Rooney aliechukua wadhifa huo kwa mara ya kwanza baada ya kuichezea England mara 57, iliwakosa karibu Nyota wake 9 kwenye mechi hiyo huku Brazil ikiwa na Kikosi imara.
Brazil: Julio Cesar, Maicon, Lucio, Thiago Silva, Michel Bastos, Felipe Melo, Silva, Elano, Kaka, Nilmar, Luis Fabiano.
AKIBA: Doni, Dani Alves, Luisao, Juan, Aurelio, Josue, Lucas, Alex, Julio Baptista, Robinho, Carlos Eduardo, Hulk.
England: Foster, Brown, Upson, Lescott, Bridge, Wright-Phillips, Barry, Jenas, Milner, Rooney, Bent.
AKIBA: Green, Cahill, Warnock, Huddlestone, Crouch, Defoe, Young, Hart.
No comments:
Post a Comment