Monday 16 November 2009

Van Persie nje wiki 6!!!
Arsenal imetangaza kuwa Staa wao toka Uholanzi Robin van Persie atakuwa nje ya uwanja kwa wiki zinazokadiriwa kuwa 6 ili kuuguza enka yake aliyoumizwa kwenye mechi ya kirafiki kati ya Uholanzi na Italia Jumamosi iliyopita.
Awali ilidhaniwa Van Persie anaweza kuwa nje ya uwanja kwa miezi mitatu lakini Arsenal imesema uchunguzi wa Madaktari umebaini hakuumizwa sana kama ilivyoogopwa awali.
Uswisi Mabingwa wa Dunia Vijana Chini ya Miaka 17!!!
Nigeria 0 Uswisi 1
Uswisi jana waliwaliza Nigeria nyumbani kwao Abuja baada ya kuwafunga bao 1-0 katika Fainali ya Kombe la Dunia kwa Vijana Chini ya Miaka 17.
Bao la ushindi kwa Uswisi lilifungwa na Haris Seferovic dakika ya 63 mbele ya Mashabiki wa Nigeria wapatao 60,000.
Hilo ni pigo kubwa kwa Nigeria ambao wameshawahi kutwaa Kombe hilo mara 3.
Katika mechi ya awali ya kutafuta Mshindi wa 3, Spain iliishinda bao 1-0 Colombia Mfungaji akiwa Isco kwenye dakika ya 75.

No comments:

Powered By Blogger