Thursday 1 October 2009

Man U 2 Wolfsburg 1
Owen acheza dakika 20 tu, aumia!!!
Manchester United wakiwa nyumbani Old Trafford walijikuta wako nyuma kwa bao 1-0 bao lilofungwa dakika ya 56 kwa kichwa na Edin Dzeko lakini wakajitutumua na kusawazisha dakika 3 baadae pale frikiki ya Ryan Giggs ilipobabatiza ukuta wa Wolfsburg na kumhadaa Kipa wao.
Mshambuliaji wa Man U Michael Owen alianza mechi ya jana lakini alidumu dakika 20 tu na ilibidi atolewe nje baada ya kujitonesha paja aliloumia wiki iliyokwisha na Dimitar Berbatov akaingia badala yake.
Kutolewa kwa Owen ni pigo kwa Mchezaji huyo anaelilia namba Kikosi cha Timu ya England hasa kwa kuwa Kocha wa England Fabio Capello alikuwa shuhuda wa mechi hiyo.
Zikiwa zimesalia dakika 12, Giggs, baada ya hekaheka za Rooney, alimtengeneza mpira murua Michael Carrick aliefumua shuti na kuipa ushindi Manchester United.
Kwa ushindi wa jana, Man U wanaongoza Kundi B wakiwa na pointi 6, Wolfsburg na CSKA Moscow ni wa pili wakiwa na pointi 3 kila mmoja. Besiktas yuko mkiani bila pointi.
Mechi zinazofuata Kundi hili ni Oktoba 21 kati ya CSKA Moscow v Man U NA Wolfsburg v Besiktas.
Apoel Nicosia 0 Chelsea 1
Katika mechi mbili za UEFA CHAMPIONS LEAGUE za Kundi ambazo Chelsea wameshazicheza, Mshambuliaji Nicolas Anelka ndie mkombozi kwa kuifungia bao moja na la ushindi katika mechi hizo.
Mechi ya kwanza Anelka aliifunga FC Porto na jana huko Cyprus Anelka alipachika bao moja na la ushindi.
Kwa ushindi wa jana, Chelsea wanaongoza Kundi lao kwa pointi 6, FC Porto wa pili akiwa na pointi 3 na wamwisho ni Apoel Nicosia na Atletico Madrid waliofungana wakiwa na pointi moja moja.
Mechi zinazofuata ni Chelsea v Atletico Madrid na FC Porto v Apoel Nicosia.
Wakati Fergie akimsifia Giggs, Ancelotti akasirishwa na Chelsea yake!!!
Sir Alex Ferguson amemminia sifa Veterani wake Ryan Giggs kwa kusababisha ushindi wa jana dhidi ya Wolfsburg alipofunga bao la kwanza na la kusawazisha na kutengeneza la pili na la ushindi.
Ferguson amesema: “Giggs ni tishio! Amepata sifa nyingi miaka yake yote ya uchezaji na sijui utaongeza nini! Kitu cha kushangaza ni kuwa bado anaonekana mbichi!!”
Giggs, anaetimiza miaka 36 mwezi ujao, jana alifunga goli lake la 150 na pia kuungana na Raul wa Real Madrid kwa kuwa Wachezaji pekee waliofunga mabao katika misimu 14 ya UEFA waliyocheza.
Na huko Chelsea, licha ya ushindi wa ugenini wa bao 1-0 walipoifunga Apoel Nicosia, Meneja wa Chelsea Carlo Ancelotti amekasirishwa na uchezaji hafifu wa Timu yake na imedaiwa aliwabatukia Wachezaji wake baada ya mechi.
Chelsea wikiendi iliyokwisha walifungwa 3-1 kwenye Ligi Kuu na Wigan na jana ulikuwa ndio mchezo wao wa kwanza baada ya kipigo hicho na mechi inayofuata ni ile ‘Ze Bigi Mechi” Jumapili watakapovamiwa na Liverpool Stamford Bridge kwenye mechi ya Ligi Kuu.
Ancelotti amesema: “Sikuridhika. Nataka Chelsea icheze vyema. Nataka wadhibiti, wacheze kwa moyo. Lazima tubadilike.Matokeo ni mazuri lakini uchezaji mbovu!”
Real 3 Marseille 0
Mabao ya kipindi cha pili ya Wachezaji wa bei mbaya, Ronaldo [mawili] na Kaka [moja], yaliwapa ushindi wa 3-0 juu ya Marseille ya Ufaransa ambayo ilicheza mtu 10 nusu saa ya mwisho baada ya Souleymane Diawara kuonekana kumchezea faulo Ronaldo na kutolewa nje.
Faulo hiyo iliipa Real penalti ambayo Kaka aliifunga.
MATOKEO MECHI ZA Jumatano, Septemba 30:
AC Milan 0 v FC Zurich 1
Apoel Nicosia 0 v Chelsea 1 
Bayern Munich 0 v Juventus 0
Bordeaux 1 v Maccabi Haifa 0
CSKA Moscow 2 v Besiktas 1
FC Porto 2 v Atletico Madrid 0
Manchester United 2 v Wolfsburg 1 
Real Madrid 3 v Marseille 0
MECHI ZIJAZO ZA UEFA CHAMPIONS LEAGUE
Jumanne, 20 Oktoba 2009
AZ Alkmaar v Arsenal
Barcelona v Rubin Kazan
Debrecen v Fiorentina
Inter Milan v Dynamo Kiev
Liverpool v Lyon
Olympiakos v Standard Liege
Rangers v Unirea Urziceni
VfB Stuttgart v Sevilla
________________________________________
Jumatano, 21 Oktoba 2009
Bordeaux v Bayern Munich
CSKA Moscow v Man United
Chelsea v Atletico Madrid
FC Porto v Apoel Nicosia
FC Zurich v Marseille
Juventus v Maccabi Haifa
Real Madrid v AC Milan
Wolfsburg v Besiktas
________________________________________
Jumanne, 3 Novemba 2009
AC Milan v Real Madrid
Apoel Nicosia v FC Porto
Atletico Madrid v Chelsea
Bayern Munich v Bordeaux
Besiktas v Wolfsburg
Maccabi Haifa v Juventus
Man United v CSKA Moscow
Marseille v FC Zurich________________________________________
Jumatano, 4 Novemba 2009
Arsenal v AZ Alkmaar
Dynamo Kiev v Inter Milan
Fiorentina v Debrecen
Lyon v Liverpool
Rubin Kazan v Barcelona
Sevilla v VfB Stuttgart
Standard Liege v Olympiakos
Unirea Urziceni v Rangers

No comments:

Powered By Blogger