Thursday 1 October 2009


EUROPA LIGI: FC BATE Borisov 1 Everton 2
Everton waliokuwa ugenini huko Minsk, Belarus bila ya Wachezaji wao 7 wa Kikosi cha kwanza waliokosekana kwa kuwa majeruhi au wagonjwa walijikuta wako nyuma kwa bao moja hadi mapumziko lakini mabao ya kipindi cha pili ya Marouane Fellaini na Tim Cahill yaliwapa ushindi wa bao 2-1 kwenye mechi ya Kundi lao kwenye EUROPA LIGI.
Mechi nyingine za Timu za Uingereza zinazochezwa leo na zilizoanza muda si mrefu uliopita ni kati ya Celtic v Rapid Vienna na Fulham v Basle.
Rooney: Wanatuponda bureeee!!!!!
Wayne Rooney amesistiza Manchester United sasa inaanza kuwaonyesha waliokuwa wanaiponda kwa kudai kuwa kuondoka kwa Cristiano Ronaldo kumewaathiri kwamba wao bado imara kwa vile wanaongoza Ligi Kuu England na pia wako juu kwenye Kundi lao kwenye mashindano ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE baada ya kushinda mechi mbili ya kwanza ikiwa ugenini huko Uturuki walipoifunga Besiktas 1-0 na ya pili ile ya jana walipowabwaga Mabingwa wa Ujerumani Wolfsburg Old Trafford mabao 2-1.
Rooney amesema: “Binafsi nadhani tumelaumiwa bure! Ndio tulifungwa na Burnley lakini tumeshinda mechi zote nyingine!”
Rooney amekiri kuondoka kwa Ronaldo ni pengo lakini amesema Man U sasa wanacheza soka ya staili tofauti kwa vile msimu uliopita mipira ilichezwa kupitia Ronaldo lakini sasa Timu inacheza kitimu na Wafungaji ni wengi.
Mpaka sasa Rooney ndie anaeongoza kwa ufungaji ndani ya Man U kwa kupachika bao 6.
Wakati huohuo, Meneja wa Man U Sir Alex Ferguson ameahidi kumchezesha golini Kipa Ben Foster siku ya Jumamosi mechi ya Ligi Kuu huko Old Trafford watakapokutana na Sunderland. Jana, katika mechi na Wolfsburg, langoni alikuwa Kipa Tomasz Kuszczak.

No comments:

Powered By Blogger