Friday 2 October 2009

LIGI KUU ENGLAND :
RATIBA
[saa za bongo]
Jumamosi, Oktoba 3
[mechi zote saa 11 jioni isipokuwa ikitajwa]
Bolton v Tottenham
Burnley v Birmingham
Hull City v Wigan
Manchester United v Sunderland [saa 1 na nusu usiku]
Wolverhampton v Portsmouth
Jumapili, Oktoba 4
Arsenal v Blackburn [saa 9 na nusu mchana]
Chelsea v Liverpool [saa 12 jioni]
Everton v Stoke City [saa 11 jioni]
West Ham v Fulham [saa 11 jioni]
Jumatatu, Oktoba 5
Aston Villa v Man City
Keegan ashinda Kesi, kulipwa Pauni Milioni 2 fidia kwa kutimuliwa Newcastle!!
Meneja wa zamani wa Newcastle ameshinda kesi kwenye Tume ya Ajira aliyodai hakutendewa haki pale alipoandoka Newcastle na sasa Newcastle itabidi imlipe fidia ya Pauni Milioni 2 pamoja na riba.
Tume hiyo ilikubaliana na Keegan kuwa Klabu ilikiuka mkataba na Keegan pale ilipoamua kumnunua Kiungo kutoka Uruguay Ignacio Gonzalez bila ridhaa ya Keegan na hapo ndipo Keegan aliamua kung’atuka Newcastle Septemba 2008.
Keegan alijiunga na Newcastle Januari 2008 kuchukua nafasi ya Sam Allardyce alietimuliwa.
Owen kurudi uwanjani mapema!!
Mshambuliaji wa Manchester United Michael Owen anategemewa kurudi uwanjani mapema kuliko ilivyotegemewa awali baada ya Wataalam kuthibitisha maumivu yake ya paja si mabaya kama ilivyoogopwa.
Owen alicheza dakika 20 tu za kwanza kwenye mechi ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE siku ya Jumatano Man U walipoifunga Wolfsburg 2-1.
Sir Alex Ferguson amethibitisha Owen anaweza kucheza mechi ya Ligi Kuu na Bolton tarehe 17 Oktoba na pia alisema Kipa Edwin van der Sar, alievunjika kidole cha mkono, na Beki Chipukizi Rafael da Silva, aliefanyiwa upasuaji begani, wote wamepona na wako mazoezini ingawa hawategemewi kucheza mechi ya kesho ya Ligi Kuu na Sunderland itakayochezwa Old Trafford.
Rooney kutocheza mkewe akijifungua!!
Straika nyota wa Manchester United, Wayne Rooney, amesema kwake familia yake ni muhimu kupita soka na hivyo hatocheza mechi siku mkewe akijifungua mtoto wao wa kwanza.
Mkewe Rooney, Coleen, ni mja mzito na anatarajiwa kujifungua mtoto wao wa kwanza tarehe 24 Oktoba, siku ambayo ndiyo bethidei ya Rooney, na tarehe hiyo ni siku 3 tu baada ya Manchester United kucheza Moscow, Urusi na CSKA Moscow kwenye UEFA CHAMPIONS LEAGUE.
Rooney amesema: “Ikitokea kitu kabla ya kusafiri kwenda Moscow basi sitoenda kucheza lakini kama mambo ni kama tunavyotegemea ntacheza tu!”

No comments:

Powered By Blogger