Saturday 3 October 2009

TATHMINI MECHI ZA LIGI KUU WIKIENDI HII: “Ze Bigi Mechi” ni Jumapili Chelsea v Liverpool!!!
Chelsea watakuwa wenyeji wa Liverpool Uwanjani Stamford Bridge katika “Ze Bigi Mechi” siku ya Jumapili.
Chelsea walianza Ligi vizuri mno lakini wikiendi iliyopita walipata kipigo kitakatifu mikononi mwa Wigan walipokung’utwa 3-1 mechi ambayo ilimfanya Nahodha wa Chelsea John Terry kuwalaumu Wachezaji wenzake na pia kumfanya Meneja wao Carlo Ancelotti ajisahau kwa hasira na kuzungumza na Wachezaji wake Kitaliano.
Vinara wa Ligi Kuu na Mabingwa Watetezi Manchester United watawakaribisha Sunderland Old Trafford, Blacburn Rovers watasafiri hadi Emirates Stadium kucheza na Arsenal, West Ham na Fulham watacheza katika “dabi” ya London.
Ingawa Chelsea walipigwa kwenye Ligi Kuu wikiendi iliyopita walirudia tena ushindi pale walipocheza katikati ya wiki ugenini huko Cyprus na kuifunga Apoel Nicosia bao 1-0 kwenye UEFA CHAMPIONS LEAGUE.
Wapinzani wa Chelsea Jumapili hii, Liverpool, walionja joto ya jiwe walipotandikwa 2-0 na Fiorentina huko Italia kwenye UEFA CHAMPIONS LEAGUE siku ya Jumanne.
Mechi hiyo ilimfanya BosI wao Rafa Benitez kuiponda timu yake na kuwaambia walicheza mchezo mbovu ingawa aliahidi Jumapili watabadilika.
Chelsea watacheza mechi ya Jumapili kwa kujiamini hasa kwa vile hawajapoteza mchezo wa Ligi hapo kwao Stamford Bridge tangu Novemba, 2008 ingawa safari hii watapambana na Straika anaeng’ara sana Fernando Torres.
Lakini jambo la kutia wasiwasi kwa Liverpool ni udhaifu wa ngome yao hasa Jamie Carragher anaeonyesha kupwaya mno msimu huu.
Jumamosi, Tottenham wanasafiri hadi Kaskazini Magharibi mwa England kwenda Uwanja wa Reebok kucheza na Bolton Wanderers iliyo chini ya Meneja Gary Megson ambae ameifanya timu yake katika mechi tatu za hivi karibuni kuvuna pointi 7. Tottenham ambao kawaida hawafanyi vizuri uwanjani Reebok watajipa moyo kidogo hasa kwa kuanza kampeni yao ya Ligi msimu huu kwa mguu mzuri mno.
Wolverhampton Wanderers watapambana na Portsmouth walio mkiani na ambao wamefungwa mechi zao zote za Ligi msimu huu.
Burnley na Birmingham City, timu zilizopanda Daraja msimu huu, zitakutana uso kwa uso na Burnley watajifariji mno kwa takwimu ya kuwa na pointi 9 ambazo zote wamezipatia Uwanja wa nyumbani Turf Moor ikiwa pamoja na kuzifunga Manchester United na Everton.
Hull City, timu inayozama kwa spidi kali msimu huu, itawakaribisha KC Stadium Wigan ambao ndio wababe wa Chelsea waliyoifunga mechi yao ya mwisho ya Ligi goli 3-1. Msimu uliokwisha katika mechi kama hii, Wigan walibandika Hull mabao 5-0.
Mabingwa Manchester United wataialika Sunderland Old Trafford huku Veterani wao Ryan Giggs akiwa ndie Staa wao kwa hivi karibuni. Sunderland iko chini ya Mchezaji wa zamani wa Mabingwa hao Steve Bruce.
Jumapili Arsenal wanacheza na Blackburn Emirates Stadium ikiwa ni mechi ya kwanza kwa Arsene Wenger tangu kuingia kwa mwaka wake wa 14 akiwa na Arsenal ambayo ni rekodi katika historia ya Klabu hiyo kwa kuwa ni Meneja aliedumu muda mrefu zaidi.
Mechi ya ushindani ni ile ‘dabi’ ya Timu za London West Ham v Fulham Klabu ambazo msimu huu zinasuasua na ziko chini kwenye msimamo wa Ligi zote zikiwa zimefungwa mechi 4 katika 5 walizocheza mwisho.
Huko Goodison Park, Wenyeji Everton wakiwa na Mshambuliaji wao Luis Saha ambae yuko kwenye fomu watapambana na Stoke City. 
FIFA U20 WORLD CUP EGYPT 2009:
Ghana, Germany, Korea na Uruguay zaingia Raundi ya Pili!!
Kipigo cha Cameroun chaibeba Nigeria kusonga mbele kama Mshindi wa 3!!!
Cameroun ilichapwa mabao 3-0 na Germany na hivyo kuipa mwanya Nigeria iliyomaliza Kundi lake nafasi ya 3 kuingia kama mmoja wa Washindi wa 3 bora na kuibwaga Cameroun.
Katika Kundi la Cameroun, Germany ndie Mshindi wa 1 na South Korea wa pili.
Ghana amemaliza Kundi D akiwa Mshindi wa kwanza na Uruguay wa pili.
Washindi wa Kwanza na wa Pili kila Kundi wanasonga mbele pamoja na Washidi wa nafasi ya tatu bora 6 kati ya Timu 8 zitakazomaliza nafasi hiyo.
Mpaka sasa Timu zilizoingia Raundi ya Pili ni:
KUNDI A: Egypt, Paraguay
KUNDI B: Spain, Venezuela, Nigeria
KUNDI C: Germany, South Korea
KUNDI D: Ghana, Uruguay
KUNDI E: Brazil, Czech Republic
KUNDI F: UAE na nyingine kujulikana leo.
MATOKEO MECHI ZA JANA Ijumaa, Oktoba 2:
Germany 3 v Cameroun 0
Uzbekistan 1 v England 1
South Korea 3 v USA 0
Uruguay 2 v Ghana 2
MECHI ZA LEO Jumamosi, Oktoba 3:
-South Africa v Honduras
-Hungary v UAE
-Australia v Brazil
-Costa Rica v Czech Republic
RATIBA LIGI ZA ULAYA:
BUNDESLIGA:
MATOKEO: Ijumaa, Oktoba 2:
Schalke 04 2 v Eintracht Frankfurt 0
RATIBA:
Jumamosi, Oktoba 3
Bayer 04 Leverkusen v FC Nurnberg
Bayern Munich v FC Koln
Hannover v SC Freiburg
VFL Bochum v VfL Wolfsburg
FSV Mainz v TSG Hoffeinheim
Borussia Munchen Gldbach v VB Borussia Dortmund
Jumapili, Oktoba 4
VfB Stuttgart v SV Werder Bremen
Hertha Berlin v Hamburger SV
ITALIA SERIE A:
Jumamosi, Oktoba 3
As Bari v Catania
Inter Milan v Udinese
Jumapili, Oktoba 4
Atalanta v AC Milan
Bologna v Genoa
AS Roma v Napoli
Sampdoria v Parma
Siena v Livorno
Cagliara v Chievo Verona
Fiorentina v SS Lazio
Palermo v Juventus
SPAIN LA LIGA:
Jumamosi, Oktoba 3:
Cd Tenerife v Deportivo La Coruna
FC Bacerlona v UD Almeria
Atletico de Madrid v Real Zaragoza
Jumapili, Oktoba 4
Real Valladolid v Athletic de Bilbao
Villareal v Espanyol
Sporting Gijon v Real Mallorca
Getafe v Osasuna
Xerez CD v Malaga CF
Racing de Santander v Valencia
Sevilla v Real Madrid

No comments:

Powered By Blogger