Thursday, 1 October 2009

Wenger aweka rekodi Arsenal
Sasa Arsene Wenger ndie Meneja aliedumu muda mrefu katika historia ya Arsenal baada ya kuifikia na kuipita rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na George Alison ambae alikuwa Meneja wa Arsenal kwa miaka 13 hadi mwaka 1947.
Wenger, ambae ni Mfaransa, alianza kazi ya Umeneja Arsenal mwaka 1996 akitokea Japan.
Makamu Mwenyekiti wa zamani wa Arsenal, Mike Dean, ndie aliemleta Wenger hapo Arsenal na wakati huo watu wengi walishangazwa na hatua hiyo hasa kwa vile Wenger alikuwa hatambuliki huko Uingereza.
Lakini katika msimu wake wa kwanza tu na Arsenal, Wenger alimudu  kuifanya Arsenal itwae Ubingwa na kunyakua Kombe la FA.
Dean anaeleza: "Tulimchukua huku Klabu kubwa kama Bayern Munich zilikuwa zikimtaka. Alifanya mabadiliko makubwa alipoingia Arsenal. Alibadili hali za Wachezaji kuanzia ulaji, mazoezi na maisha yao! Yeye ni msomi! Amesomea Udaktari, Uchumi na ana ufahamu wa mambo mengi!!"

Wachezaji Portsmouth hawajalipwa Mishahara!!
Klabu ya Portsmouth imetangaza kuwa Wachezaji na Wafanyakazi
wa Klabu hiyo watalipwa Mishahara yao katika masaa 24 yajayo baada ya Mmiliki mpya wa Klabu hiyo kutoka Dubai Sulaiman al Fahim kutuma fedha kwa lengo hilo.
Klabu hiyo iliyokuwa ikikabiliwa na matatizo ya kifedha hivi karibuni ilinunuliwa na Tajiri huyo kutoka Dubai ambae pia ndie aliesuka na kushughulikia ununuzi wa Manchester City kwa Familia moja ya Koo ya Kifalme kutoka Abu Dhabi.
Sulaiman al Fahim yeye binafsi ndie alieinunua Portsmouth.
FIFA U20 WORLD CUP EGYPT 2009:
MATOKEO MECHI ZA JANA Jumatano, Septemba 30:
Australia 0 Costa Rica 3
Brazil 0 Czech Republic 0
Hungary 4 South Africa 0
UAE 1 Honduras 0
MECHI ZA LEO Alhamisi, Oktoba 1:
Trinidad & Tobago v Paraguay
Italy v Egypt
Venezuela v Spain
Tahiti v Nigeria

No comments:

Powered By Blogger