Sunday 29 August 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

LIGI KUU kusitishwa hadi Septemba 11
Mechi za Ligi Kuu England zitakuwa mapumzikoni hadi Septemba 11 ili kuzipisha Mechi za Kimataifa za Nchi za Ulaya kugombea kufuzu Fainali za EURO 2012 ambazo zitachezwa Wikiendi hii na katikati ya Wiki ijayo.
England itaingia dimbani hapo Ijumaa Septemba 3 kucheza na Bulgaria Uwanjani Wembley Jijini London na Jumanne Septemba 7 itacheza na Uswisi.
LIGI KUU England: RATIBA inayofuata
Jumamosi, 11 Septemba 2010
[Saa 8 dak 45 mchana]
Everton v Man United
[Saa 11 jioni]
Arsenal v Bolton
Fulham v Wolverhampton
Man City v Blackburn
Newcastle v Blackpool
West Brom v Tottenham
West Ham v Chelsea
Wigan v Sunderland
Jumapili, 12 Septemba 2010
[Saa 12 jioni]
Birmingham v Liverpool
Jumatatu, 13 Septemba 2010
[Saa 4 usiku]
Stoke v Aston Villa
Villa 1 Everton 0
Leo Aston Villa, baada ya kuchapwa 6-0 na Newcastle wiki iliyopita, wamejirekebisha na kuutumia vizuri Uwanja wao Villa Park kwa kuwafunga Everton bao 1-0 katika mechi ya Ligi Kuu.
Bao la Villa lilifungwa na Luke Young dakika ya 9.
Everton walizidisha presha baada ya bao hilo lakini nguvu zao zote ziliishia kwa ama Kipa Brad Friedel, kutoa nje na mara moja kugonga mwamba baada ya shuti kali la Pienaar.
Matokeo ya mechi hii yamewafanya Villa wawe na pointi 6 kwa mechi 3 na wako nafasi ya 4 nyuma ya Chelsea, Arsenal na Man United.
Everton wao wako nafasi ya 3 toka mkiani wakiwa na pointi moja tu baada ya mechi 3.

No comments:

Powered By Blogger